Kiungo mshambuliaji wa Klabu Azam FC, Salum Abubakar ‘Sureboy’ amesema anaimani kubwa Kuwa timu yake itafika mbali kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika mwaka huu.
Sureboy alifunga bao la ufunguzi kwenye mechi yao ya ugenini dhidi ya Bidvest Jumamosi Hii ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
“Namshukuru sana Mungu Kwa ushindi wetu. Tulicheza Kwa umoja Na kwa kufuata maelekezo ya Mwalimu Ndio maana tukapata ushindi huu,” Sureboy aliuambia mtandao waSoka360
“Nimejisikia furaha kuwa mmoja wa wafungaji kwenye mechi hio. Kiufupi nilicheza Vizuri sana,”
“Bidvest ni timu nzuri ila tuliwazidi mbinu ndio maana tukapata ushindi. Naimani Azam itafika mbali, Kwa kuwa malengo yetu nikufanya vizuri.”
Azam itacheza mechi ya marudiano dhidi ya Bidvest Wits tarehe 20 mwezi huu jijini Dar es salaam.


0 comments:
Post a Comment