Monday, February 8, 2016

Abdallah 'King' Kibadeni (kushoto) na Mrage Kabange (kulia) wakuu wa benchi la ufundi la JKT Ruvu

Mshauri wa benchi la ufundi la timu ya JKT Ruvu kocha mzoefu Abdallah Kibadeni ‘King Kibadeni’ amekiri timu yake ilizidiwa na Yanga kwenye mchezo wao wa jana na kujikuta ikichezea kichapo cha magoli 4-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwenye uwanja wa taifa.
Kibadeni amesema kichapo cha magoli 4-0 kimekuja kutokana na namana ambavyo timu yake ilicheza na kushindwa kuhimili mziki mzito wa Yanga.
“Kulingana na namna tulivyocheza tulistahili kufungwa idadi kubwa ya magoli kwasababu walituzidi sana kwa mbinu za kimchezo. Wao walikuwa wakitumia uzoefu wao kutafuta magoli mengi na walipata na sisi tulishindwa kabisa kuwazuia”, amesema Kibadeni.
“Kwahiyo kilichobaki ni kujipanga maana timu zote si Simba, Yanga na Azam kwa maana timu kubwa, wachezaji wasikate tamaa na wakubali kwamba wao wako chini na wapambane kuhakikisha wanaipeleka timu mahali pale inapostahili”.
Mwisho Kibadeni alisema, inabidi JKT Ruvu ipambane kwa nguvu zote pindi inapokutana na timu zenye uwezo sawa nayo ili kuhakikisha inaibuka na ushindi na kukwepa kushuka daraja msimu huu.
JKT Ruvu ipo nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na pointi 13 sawa na timu za African Sports na Coastal Union lakini wanatofautiana wastani wa magoli ya kufungwa na kufunga.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video