Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku anataka kujiunga na Paris St-Germain au Real Madrid kuliko kwenda Manchester United (Sun), Barcelona wanamtaka kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey na beki wa Everton John Stones (Express), Arsenal wanataka kutumia pauni milioni 52 kumsajili kiungo Granit Xhaka kutoka Borussia Monchengladbach na Adrien Rabiot kutoka Paris St-Germain (Star), meneja wa Liverpool amechoshwa na kuumia kila mara kwa Daniel Sturridge na yuko tayari kumuuza mshambuliaji huyo (Mirror), meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ni miononi mwa majina yanayotajwa na wakurugenzi wa Manchester United kumrithi Louis van Gaal (Mirror), Swansea watampa nafasi Wilfried Bony ya kurejea tena katika klabu hiyo, na pia wanafikiria kumsajili kiungo wa AC Milan Nigel de Jong (Sun), Tottenham wanataka kupanda dau tena la kumsajili Saido Berahino kutoka West Brom kwa kutoa pauni milioni 20 pamoja na winga Andros Townsend (Star), Lazio walikataa dau la pauni milioni 37.6 kutoka Manchester United kumtaka kiungo Filipe Anderson mwezi Agosti mwaka jana, lakini hawakupata dau jingine tena (ESPN), Manchester United wamekataa ombi la AC Milan la kumsajili kwa mkopo Marouanne Fellaini, lakini wamesema wako tayari kumuuza kwa pauni milioni 24 (Mirror), meneja wa Manchester United Louis van Gaal hatarajii kusajili mchezaji yoyote katika dirisha la usajili la Januari (Talksport), mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski anafikiria hatma yake na mabingwa hao wa Ujerumani. Manchester United, Manchester City na Chelsea zinamtaka mchezaji huyo (Independent), Everton wanajiandaa kutoa pauni milioni 21 kumsajili winga wa Dynamo Kiev Andriy Yarmolenko (Mail), Pep Guardiola amewaambia Manchester City kuwa anamtaka kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan na beki wa kati wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte kama sehemu ya kikosi chake atakapotua Etihad (Express), wakala wa Yaya Toure ana wasiwasi na hatma ya mchezaji huyo iwapo Guardiola ataenda City. Meneja huyo alimuuza Toure mwaka 2010 alipokuwa Barcelona (Sunday Mirror), meneja wa Arsenal amedokeza kuwa usajili wa Mohamed Elniny ambao utakamilika hivi karibuni, ndio usajili pekee mwezi huu (London Evening Standard), kiungo wa Sevilla Grzegorz Krychowiak anasema anafahamu kuwa Arsenal wanamfuatilia (FourFourTwo), mshambuliaji wa Stoke City Marco Arnautovic anataka mshahara wa zaidi ya pauni laki moja kwa wiki ili aongeze mkataba wake. Kikomo cha mshahara Stoke ni pauni 70,000 kwa wiki (Observer).
Sunday, January 10, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment