Saturday, December 19, 2015

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameilezea hali ya kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha wa Chelsea kama "hali ya kuhuzunisha sana".
Mourinho alifukuzwa Alhamisi wiki hii baada ya kushuhudia Chelsea ikipoteza michezo tisa kati ya 16 iliyocheza msimu huu.
Akiwa ameshawahi kukumbana na hali kama hiyo katika msimu wake wa mwisho alipokuwa akiinoa Borussia Dortmund, Klopp ameonyesha kuhuzunishwa sana na hatua hiyo iliyochukuliwa dhidi ya Mreno huyo lakini anaamini kwamba atapata faraja kwa kipindi ambacho atakuwa nje ya soka.
"Ni hali ya kuhuzunisha sana kuona uhusiano mzuri katika ya Mourinho na Chelsea unaisha kwa namna hii," Klopp aliwaambia wanahabari.
"Namtakia Jose maisha mema huko aendako. Ni vizuri kupata mapumziko kidogo hasa baada ya kufanya mambo makubwa sana kwa kipindi kirefu bila ya kuyumba.
"Wakati mwingine mchezo wa mpira wa miguu huwa kama hivi, lakini najua kwa nini napaswa kuzungumza hili juu ya Chelsea. Nilikumbana na hali kama hii wakati nikiwa Dortmund na ni vigumu sana kukumbana na hali ambayo hukuwahi kuitegemea."
Klopp amekazia maelezo yake kwa kusema kwamba soka la England halijashuka kutokana na kufukuzwa hovyo kwa makocha.
"Hapana," alisema. "Timu zote zina wachezaji wenye uwezo mkubwa sana kwa sababu ya matumizi makubwa ya fedha. 
"Ndiyo maana unakuta matokeo mengi yanakaribiana. Na hicho ndicho kinachozidi kuisisimua Ligi kuu nchini Uingereza. Nyote mnatakiwa kuwa na umakini wa hali ya juu. Kuna nyakati chache sana ambazo unaweza kupata furaha. 

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video