Monday, December 14, 2015


Wakati zikiwa zimesalia siku zinazohesabika ili dirisha dogo la usajili wa mwezi January lifunguliwe, tayari pilikapilika za usajili zimepamba moto barani Ulaya huku kila klabu ikiwa kwenye mawindo ya kujaribu kumnasa mtu sahihi ambaye atasaidia kuipa mafanikio timu hiyo.
Hizi ni habari tano (5) ambazo zimepewa nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari vya Ulaya ikiwemo vile vya Engand.
5. Swansea City inamtaka boss wa Sanchez
Chile's head coach Jorge Sampaoli celebrates a goal by his team during a 2014 World Cup qualifying soccer match against Bolivia in Santiago June 11, 2013.   REUTERS/Ivan Alvarado (CHILE - Tags: SPORT SOCCER)
Inaripotiwa kikosi cha Swansea City kiaangalia uwezekano wa kumnyakua kocha wa Chile Jorge Sampaoli ambaye inaamika kuwa hayuko kwenye wakati mzuri na shirikisho la soka la nchi hiyo ya Amerika ya Kusini.
Sampaoli alikiongoza kikosi cha Chile kutwaa taji la Copa America majira ya kiangazi yaliyopita. Lakini kikosi cha Swansea pia kianaangalia namna ya kumnasa kocha wa zamani wa Sunderland Gus Poyet ili kuziba nafasi ya Garry Monk aliyetimuliwa siku za hivi karibuni.
4. Juventus inaongeza nguvu kwa Oscar
Usajili 1
Miamba ya Italia Juventus imerejea darajani kwa mara nyingine kujaribu kumsajili Oscar mchezaji ambaye wamekuwa wakimuwinda kwa muda mrefu. Mabingwa hao wa Serie A wamekuwa wakimfatilia mbrazil huyo kwa muda na safari hii inaamika wako tayari kulipa kiasi chohote cha pesa ili kumpata.
3. Valencia ilimtaka Giggs kabla ya kumsaini Garry Neville
Usajili 2
Ripoti kutoka Hispania zinadai kwamba wamiliki wa klabu ya Valencia walikuwa wanamtaka Ryan Giggs kabla ya kumsaini mchezaji mwenzake Garry Neville. Kwa mujibu wa ripoti hizo, Giggs alikataa offer hiyo kwasababu natarajia kurithi mikoba ya Mholanzi Lois van Gaal ambaye anamaliza mkataba wake ndani ya Manchester United mwaka 2017.
2. Cech aingia kwenye vitabu vya rekodi EPL
Usajili 3
Clean sheet aliyoipata golikipa wa Arsenal Petr Cech dhidi ya Aston Villa weekend iliopita imemfanya kufikia rekodi iliyowekwa na David James ya clean sheets 169 kwenye ligi ya EPL. Golikipa mwenzake waliyedaka nae pamoja kwenye klabu ya Chelsea Carlo Cuducini amempongeza kwa mafanikio makubwa aliyoyafikia.
1. Ancelotti kutua Bayern
Usajili 4
Kocha wa zamani wa Real Madrid na Chelea Carlo Ancelotti anahusishwa kujiunga na klabu ya Bayern Munich majira ya joto ya msimu ujao endapo Pep Guardiola ataondoka kwenye klabu hiyo.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona amekuwa akihusishwa na vilabu vya ligi ya England vya Manchester United na Manchester City.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video