Saturday, August 15, 2015

Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars kilichoweka kambi kisiwani Zanzibar kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) kinaendelea kujifua kutwa mara mbili katika viwanja wa Amaan na Fuoni kabla ya safari ya kuelekea nchini Congo – Brazzavile mwezi ujao.

Twiga Stars chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Starlets) Agosti 23  katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibari ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michezo hiyo ya Afrika (All Africa Games).

Kaijage amesema anashukuru vijana wake wanafanya mazoezi kwa morali ya hali ya juu, wachezaji wanaonekana kuyashika vizuri mafunzo yake na kumpa imani kuwa sasa kikosi chake kimeiva na anachosubiri ni mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya ili kuweza kuona uwezo wa kikosi chake kabla ya safari ya kuelekea nchini Congo-Brazzavile.

Akiongelea maendeleo ya kambi ya Twiga Stars, Mkuu wa Msafara Blassy Kiondo amesema timu ipo katika hali nzuri, wachezaji wanafanya mazoezi  kwa morali ya hali ya juu, hakuna majeruhi,  kikubwa wanachosubiri kwa sasa ni huo mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya mwishoni mwa wiki ijayo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video