Sunday, August 9, 2015

Winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa (wapili) kushoto akiwa na wachezaji wenzake wa Free State Stars

Winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa anaekipiga kwenye klabu ya Free State Stars inayoshiriki ligi kuu ya nchini South Afrika ameanza vibaya ligi hiyo kwa timu yake kupokea kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Mpumalanga Black Aces ambayo pia ni timu iliyomsajili nyota wa Yanga Kpah Sherman.

Bhongolwethu Jayiya alifunga goli pekee lililoipa Black Aces ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi kuu ya Afrika Kusini msimu wa 2015/2016 uliochezwa kwenye uwanja wa Goble Park ambao ni uwanja wa nyumbani wa Free State Stars.

Ngassa alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Free State Stars pamoja na Sthembiso Ngcobo ambaye pia ni mchezaji mpya kwenye kikosi hicho huku timu yake ikipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi lakini mambo yakawa tofauti.

Kikosi cha Free State Stars kilichoanza kwenye mchezo dhidi ya Black Aces

Kwenye mchezo huo Ngassa alioneshwa kadi ya njano dakika ya 54 na baadae dakika ya 63 alipumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Danny Venter.

Free State walishindwa kupata bao mwanzoni mwa kipindi cha kwanza wakati walipotawala mchezo kabla ya Black Aces hawajapata bao dakika ya 24 kwa shambulizi rahisi. Lehlohonolo Nonyane aliambaa na mpira kisha kupiga krosi iliyomkuta Jayiya ndani ya boksi la penati na kuukwamisha mpira wavuni.

Kama walivyoanza kipindi cha kwanza, Stars walirudi kwa kasi kipindi cha pili na ilibaki kidogo Somaeb aipatie Stars goli la kusawazisha muda mfupi baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Mnamibia huyo alipiga mpira wa adhabu ndogo uliookolewa na golikipa Jackson Mabokgwane. 

Themba Shabalala aliifungia Free State Stars goli dakika ya 74 lakini mwamuzi alilikataa kwasababu kabla hajafunga tayari alimfanyia madhambi beki wa Black Aces.

Mambo yaliendelea kuwa mabaya zaidi kwa upande wa timu ya Ngassa baada ya mwamuzi kumtoa beki wao kwa kadi nyekundu Themba Shabalala dakia ya 84 kufuatia kumuonesha kadi ya njano mara mbili.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video