Monday, July 20, 2015

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba amethibitisha kwamba yupo katika mazungumzo ya kusaini kujiunga na timu inayocheza ligi kuu ya Marekani, MLS majira haya ya kiangazi.
Licha ya kuhusishwa kutua Italia, Drogba, 37, ambaye ni mchezaji huru baada ya msimu uliopita kumalizana na Machampions wa EPL, Chelsea,  anaweza kuwafuata magwiji wenzake wa Premier League, Steven Gerrard na Frank Lampard waliotua Marekani.
Akizungumza na FCInter1908 Straika huyo amesema
"Sijui kuhusu hilo (kujiunga Inter)"
"Inter ni klabu kubwa, kama wangekuwa wamenifuata ningefikiria ofa yao, lakini kwasasa nipo katika mazungumzo na timu ya MLS".
"Ninaweza kwenda Inter kama kweli wananihitaji"
Japokuwa haijathibitika ni timu gani ya MLS Drogba anataka kwenda, Ripoti zinasema Chicago Fire ndio wanapewa nafasi kubwa ya kuinasa saini ya Muivory Coast huyo.
Kama dili hilo litakamilika, klabu itakayomsajili itakuwa imepata jembe la magoli ingawa umri umekwenda.
Drogba aliifungia Chelsea magoli 164 katika mechi 381 alizocheza na alishinda mara nne ubingwa wa ligi kuu England.
Pia alifunga penati ya mwisho mwaka 2012, Chelsea ikiichapa Bayern Munich kwa matuta katika mechi ya fainali ya Uefa Champions League na kuchukua ndoo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video