Machester United wanakaribia kumsajili beki wa Real Madrid Sergio Ramos kwenye uhamisho utakaohusisha kubadilishana wachezaji ambapo Real Madrid watalazimika kumtoa Ramos pamoja na kiasi cha pesa ili kumnasa golikipa namba moja wa Man United David de Gea.
Ramos haelewi ni kwanini Madrid wameanua kumruhusu aondoke wakati bado anamkataba wa miaka miwili na klabu hiyo lakini akawaambia kwamba, iwapo naondoka Madrid basi sehemu pekee anayotaka kwenda ni Manchester United.

Ramos aliyejiunga na Madrid kitokea Sevilla mwaka 2005 ameshatwaa mataji yote kwenye mchezo wa soka akianzia ngazi ya klabu hadi kwenye timu ya taifa.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 hana furaha kwenye klabu yake hasa kwa kitendo cha klabu hiyo kuamua kumtimua aliyekuwa kocha wao Carlo Ancelotti lakini pia kitendo cha Madrid kushindwa kumpa Euro milioni 10 kwa mwaka kwa ajlili ya kuboresha mkataba mpya.
Ramos aliamini kwamba, angeongezewa mkataba mwingine kwenye majira ya kiangazi ya msimu uliopita baada ya kuifungia timu yake goli la kusawazisha dakika ya mwisho kwenye mchezo wa fainali wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Atletico Madrid na kuisaidia timu hiyo kunyakua taji hilo kwa mara ya 10 kwenye muda wa nyongeza.

Klabu ya Barcelona imelalamika kuwa, ilipeleka ofa ya kutaka kumsajili Ramos lakini hawakujibiwa chochote na Madrid, kitendo hicho kimemchukiza pia Ramos ambaye amesema anapenda zaidi kukipiga kwenye ligi ya EPL hasa Old Trafford japo bado anawindwa na Barcelona.
0 comments:
Post a Comment