Mtandao maarufu wa Forbes.com ambao mara nyingi hutoa orodha ya watu maarufu na pesa zao, hivi sasa wametoa orodha ya wanamichezo waliolipwa pesa kwa mwaka mmoja uliopita.
Katika orodha hiyo, Floyd Mayweather ameshika namba moja kwa kukusanya kiasi cha dola za Marekani milioni 300 ambapo mshahara ni Dola milioni 285mil na endorsement ni dola Milioni 15.
Namba mbili ni Manny Pacquiao ambae amekusanya kiasi cha dola milioni 160.
Baada ya hao wawili anakuja mchezasoka, Cristiano Ronaldo ambaye amepokea kiasi cha dola milioni 79.6 ambayo ni pengo kubwa sana kutoka kwa Manny na Mayweather.
Lionel Messi yupo namba 4 na amepokea pesa kiasi cha dola milioni 73.8.
Roger Federer mcheza tennis anaingia namba 5 kwa kupokea kiasi cha dola milioni 67 na kitu kizuri ni kwamba mshahara wake ni dola milioni 9, lakini endorsement ni dola milioni 58. Orodha inaendelea kama ifuatavyo.







0 comments:
Post a Comment