Shirika la BBC limeripoti kuwa timu ya soka ya Newcastle United
imemtimua kocha wake mkuu John Carver pamoja na msaidizi wake Steve Stone.
Carver mwenye umri
wa miaka 50 alichukua nafasi ya kocha Alan Pardew aliyetimkia timu ya Crystal
Palace.
Katika michezo
ishirini aliyoiongoza timu hiyo alifanikiwa kushinda michezo mitatu.
Mkurugenzi mkuu wa
timu hiyo Lee Charnley, amesema atatafutwa kocha mpya wa kuweza kuijenga timu
hiyo upya.
Kumekua na tetesi
kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingerza Steve McClaren, anaweza
kuchaguliwa kuwa kocha mpya wa kikosi cha Newcastle United.

0 comments:
Post a Comment