Tuesday, May 19, 2015


Msimu wa pili wa mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za mtaani yajulikanayo kama SPORTS XTRA NDONDO CUP unatarajiwa kuanza mei 20 mwaka huu kwa hatua ya awali.
 
Mashindano hayo yamelazimika kuanzia hatua ya mtoano kutokana na kujitokeza kwa timu nyingi zilizoomba kushiriki baada ya mwaka jana michuano hiyo kufanya vizuri.
 
Hatua ya awali inatarajiwa kufikia tamati mwezi ujao kwa kupatikana timu 16 miongoni mwa timu 81, ambazo zitaungana na timu nyingine 16 zilizofanikiwa kuingia hatua ya mtoano mwaka jana.
Katibu wa kamati ya mashindano ya DRFA,  Daud Kanuti ambaye kimsingi ndiye mratibu wa mashindano hayo amezitaka timu shiriki kuheshimu kanuni za mashindano.
 
Kanuti pia amezungumzia changamoto ya waamuzi ambayo imekua ikibebeshwa lawama katika ligi mbalimbali kutokana na ukiukwaji wa sheria kumi na saba za soka.
 
''uzuri ni kwamba DRFA tuna waamuzi wengi na wamekua wanafanya vizuri hivyo hatuna hofu na waamuzi wetu na tunaamini watafanya vizuri"alisema 

Mashindano haya yalianzishwa mwaka jana na Clouds Media Group kupitia kipindi chake bora cha michezo cha Sports Xtra kwa lengo la kutoa nafasi kwa vijana wengi mitaani kuonesha vipaji vyao.
 
Michezo ya ufunguzi hapo kesho ni kati ya Vijibweni city dhidi ya Wakung’aza Fc uwanja wa Mizinga, na Santiago Chile dhidi ya Kisarawe Rangers pale shule ya Benjamin Mkapa.
 
Michezo mingine ni kati ya Faru Jeuri dhidi ya Kisarawe United pale airwing Ukonga, na Sindano Fc na No Star uwanja wa Kinesi Sinza

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video