Klabu ya Simba imeshindwa kufikia makubaliano na mshambuliaji wa JKT Mgambo, Malimi Busungu baada ya kuahidi kumlipa dau la shilingi milioni 20 huku yeye akihitaji kulipwa shilingi milioni 40 ili asaini kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi.
Malimi kwa sasa yupo kambini na timu ya taifa 'Taifa Stars' kwa ajili ya maandalizi ya kufuzu michuano ya fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Misri.
Hata hivyo habari zilizopo ni kwamba, pande hizo mbili zitaketi tena kwa mara nyingine kwa maafikiano mengine pindi mchezaji huyo atakapomaliza kuitumikia timu ya Taifa.
0 comments:
Post a Comment