Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KINARA wa mabao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Simon Msuva, amefuata nyayo za winga mwenzake, Mrisho Ngasa baada ya leo kutua Afrika Kusini kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Orlando Pirates.
Taarifa ambazo mtandao huu umezipata kutoka kwa watu wa karibu na Msuva, zimeeleza kuwa nyota huyo aliyekulia katika klabu ya Azam FC, ameondoka jijini Dar es Salaam leo kwenda Afrika Kusini kujaribu bahati yake ya kukipiga katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro, amekiri Pirates walileta mwaliko wa majaribio kwa ajili ya Msuva, lakini wakamuambia asubiri msimu huu wa VPL umalizike.
“Ninajua kuna hiyo safari, ila aliambiwa asuburi amalize ligi atakwenda, kama amekwenda bila ruhusa atakuwa amefanya makosa, ”amesema Muro.
Msuva, mchezaji dansi wa zamani wa Kundi la THT, ameng'ara na kikosi cha Mdachi Hans van der Pluijm cha Yanga ambacho tayari amekipa ubingwa wa VPL msimu huu, huku akiongoza safu ya wafumania nyavu hatari msimu huu akiwa na mabao 17 akifuatiwa na mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita, Amissi Tambwe wa Yanga pia mwenye mabao 14.
Endapo winga huyo akifuzu majaribio 'Sauzi, ataungana na Ngasa ambaye inadaiwa kuwa tayari ameshasaini mkataba wa kuitumikia Free States ya nchini humo.

0 comments:
Post a Comment