Thursday, May 28, 2015



NIMEPITIA Ukurasa wa Simba Platnum Supporters kwenye ukurasa wa facebook na kukutana na posti hii ambayo haijataja jina la mwandishi.
Lakini bila shaka ni shabiki na mwanachama wa Simba ambaye ameamua kuandika hisia zake kuhusu mchezaji mwenye kipaji kikubwa, Ramadani Singano.
Singa na Simba wapo kwenye mgogoro wa kimkataba;

Ujumbe wenyewe huu hapa chini;

 "Mwanzoni mwa mwaka 2013,,Simba iliyokuwa na mafundi kama kina Haruna Moshi ’Boban ’ ilivunjwa makusudi na uongozi uliyokuwepo wakati huo, ikiwa na lengo la kuwapa nafasi vijana waliokuwa hatari katika timu B kipindi hicho ambayo ilikuwa ikinolewa na nahodha wa zamani wa Simba Sc Seleman Matola. .....
Kuondoka kwa baadhi ya wachezaji kipindi hicho kama Abdallah Juma ,Paul Ngalema nk ilikuwa ni jambo si la kawaida kwa kuwa Simba ilijivika mabomu ya kwenda na watoto wa Simba B!
Kikosi hicho ambacho kilifanya maajabu katika mashindano ya Super 8Banc ABC, kilitoa matunda mazuri sana, ,,Abdallah Seseme, Said Ndemla, Wilium Lucian Gallas, Ramadhan Kiparamoto ,Waziri Omary, Haruna Chanongo, Hassan Hatibu (Captain ) wakati huo ,Hassan Isihaka, Rashid, Mkoko ,Ramadhani Singano (Messi ),Jonas Mkude, Abuu Hashim, ,,,,,walianza kuonekana ........
Miezi kadhaa mbele Simba iliamua kuwapa mikataba mipya vijana hawa ,ikiwa na lengo la kuitetea klabu katika mashindano mbalimbali, ,,,Baadhi yao waliweza na wengine walichemsha, waliochemsha waliruhusu maigizo mapya na walioweza walipambana!
Mmoja kati ya wachezaji waliopambana kikweli kuitetea Simba Sc ni Ramadhani Singano ,,,kinda hili ambalo limefanya mambo makubwa sana ikiwemo kuipa Simba Sc, Kombe la Mapinduzi alikuwa hodari kweli!
Masaa machache yaliyopita, Rama akiwa anahojiwa na media fulani amefunguka mambo mazito kuhusu uongozi wa Simba SC ,sitaki kuamini kuwa Rama hafahamu kipi anachozungumza. ...moja ya kitu alichozungumzia ni kuhusu mkataba wake kuchezewa, ,mkataba wa Rama anadai kuwa ni miaka miwili ,lakini mkataba uliopelekwa TFF ni wa miaka mitatu .......
Sahau kuhusu mkataba ......mchezaji huyu mwenye kipaji cha hali ya juu ametanabaisha kuwa baadhi ya vipengele katika mkataba wake vimechezewa ........bonasi yake ya 25% hakuwahi kupata .....pango ya nyumba hakuwahi kupewa ..ni hali nzito ...
Katika kipindi hiki cha usajili kuna mambo mengi kweli ,,huwezi kufahamu yupi mkweli lakini Ramadhani Suzanna Singano ameamua kuwapeleka viongozi wake kwenye mahakama ya ’media ’
Ikumbukwe kuwa wakati Simba Sc inawapandisha vijana hawa ilijitahidi kuwahudumia kwa hali na mali ....kitendo cha kina Mafundi kama Mwinyi Kazimoto kuzungushwa ili vitoto vicheze matokeo yake ndio haya .......Rama amefanya sahihi kwa mawazo yake lakini hayupo sahihi kwa mustakabali wa soka lake ....
Simba Sc ni zaidi ya Ramadhani Singano,Simba Sc ni zaidi ya Hans Pop au Evance Aveva ......simuoni tena Ramadhani Singano akiucheza ule ule mpira wake ndani ya Simba Sc ..."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video