MBEYA City fc wamekufa goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyopigwa uwanja wa sokoine jioni ya leo.
Goli pekee la ushindi la Prisons limefungwa na Lugano Mwangama kwa mkwaju wa penalti dakika ya 90.
Baada ya mechi hiyo hali ya uwanja wa Sokoine haikuwa shwari kutokana na baadhi ya mashabiki wa Mbeya City kuchukizwa na matokeo hayo wakidai walihitaji ushindi.
Beki wa Mbeya City, Juma Nyoso (kushoto) akimtuliza kipa wake ambaye alilia sana baada ya kufungwa
0 comments:
Post a Comment