Thursday, May 14, 2015

Nonga (kulia)
MSHAMBULIAJI wa kutumainiwa wa Mbeya City FC, Paul Nonga amesema ana uhakika asilimia  mia kuwa atakuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
 Nonga amekaririwa na Tovuti ya Mbeya City akisema  kuwa licha ya kuwepo kwa ofa nyingi kutoka timu mbalimbali   zinazohitaji huduma yake  lakini anataka kubaki City kwa sababu ana furaha na maisha kwenye timu hiyo.
“Ndiyo hata kabla ya msimu  kumalizika kulikuwa na ofa  nyingi kutoka timu mbalimbali ambazo zilionesha nia ya kutaka huduma yangu,binafsi nashukuru hilo kwa sababu inaonesha  kazi yangu inakubalika, tayari  nimeshafanya mazungumzo na City na yako sehemu nzuri, kifupi hakuna shaka tena juu ya mustakabli wangu ndani ya kikosi,nia yangu ni kubaki hapa kwa misimu mingi zaidi, nina furaha na maisha ya hapa” alisema Nonga.
Akiendelea zaidi Nonga aliweka wazi kuwa ana shauku kubwa ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara akiwa na kikosi cha City  huku pia akitaka kulifuta deni la michuano ya kimataifa  kwa kikosi hiki anahisi bado anadaiwa.
“Natamani kutwaa ubingwa wa ligi nikiwa na City, hili linawezekana  tumeshiriki ligi misimu miwili kwa mafanikio, nadhani  huu ni wakati wetu sasa imani yangu kubwa timu itakuwa bora zaidi msimu ujao jambo ambalo linanisukuma kuona tunanafasi ya kutwaa ubingwa alisema Nonga.
kuhusu michuano ya kimataifa  Nonga aliyemaliza msimu akiwa amepachika wavuni mabao 4  alisema kuwa bado anahisi deni kubwa  kutoka kwa kwa mashabiki wa City ambao wana kiu kubwa ya kuona timu yao inafungua ramani nyingine kwenye michezo ya kimataifa.
“Nahisi bado nina deni kubwa kwa mashabiki wa City, ndiyo tumefanya vizuri kwenye ligi  kwa misimu miwili na mashabiki wamekuwa na furaha kwenye hilo lakini bado hatujaka kiu yao ya kushangilia timu kwenye michuano ya kimataifa  ndiyo maana nataka kubaki hapa ili nilipe deni hilo” alimaliza Nonga.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video