Thursday, May 7, 2015

Pep Guardiola na Thomas Muller wakirushiana maneno baada ya Muller kufanyiwa mabadiliko huku zikiwa zimebaki dakika 10 mpira kumalizika.
Guardiola amepata wakati mgumu sana aliporejea Nou Camp wakati timu yake ya Bayern ilipofumuliwa vibaya na Barcelona
Muller na Guardiola wakiendelea kurushiana maneno kabla ya kwenda kukaa kwenye bechi lake.
Guardiola anaelekea kumaliza msimu wa pili akiwa na Bayern huku akiwapa ubingwa wa Bundesliga mara mbili, lakini akiwa ameshindwa kuwapa ndoo ya Ulya kwa mara nyingine tena.
Guardiola ambaye ni raia wa Uhispania alionekana akikwaruzana na Muller katika eneo lake la kujidai baada ya kumfanyia mabadiliko mshambuliaji huyo raia wa Ujerumani.
Akiongelea suala hilo, mchambuzi wa kituo cha runinga cha Sky Sports, Redknapp alisema: 'Guardiola yupo kwenye klabu ambayo muda mwibgi upo katika presha sana,endapo unapoteza mchezo wowote ule.'
'Alipoichukua timu kutoka kwa Jupp Heynckes, wote tulihisi kuwa ilikuwa ni ndoto kuichukua klabu iliyotoka kubeba kombe. 
Lakini mpaka sasa bado hajafanya lolote kubwa. Inaonekana ndio kwanza anarudisha nyuma.'
Jamie Redknapp (wa pili kutoka kulia) akiwa katika studio ya Sky pamoja na Jamie Carragher (kushoto) na Thierry Henry (wa pili kutoka kushoto)
Redknapp aliongeza: 'Ugumu alionao kwa sasa ni kwamba wachezaji kama  Philipp Lahm na Bastian Schweinsteiger wanonekana kuchoka kutokana na umri,  Xabi Alonso naye umri umemtupa mkono. 
'Unapoichukua timu ambayo imetoka kubeba kombe, inakupa wakati mgumu sana. Ana vitu vingi vya kufanya ili kuijenga timu upya, na kwa presha hii aliyonayo itakuwa vigumu sana kwake kwa sasa'
Heynckes akisherehekea na Manuel Neuer katika uwanja wa Wembley, Guardiola bado hajawatimizia alichokifanya Heynckes Ulaya.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video