Sunday, April 5, 2015



'Mara tu baada ya kumalizika kwa mechi yao ya marudiano waliyolala 1-0 dhidi ya FC Platinum nchini Zimbabwe, kikosi cha Yanga kilipanda ndege na kurejea Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.'

BAADA ya kufanya kweli kimataifa, mabingwa mara 24 wa Tanzania, Yanga SC kesho asubuhi wanaingia kambini jijini Dar es Salaam kujiweka sawa kabla ya kuwavaa Wagosi wa Kaya, Coastal Union FC katika mechi ya Ligi Kuu ya Bara itakayochezwa Uwanja wa Taifa Jumatano.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, ameuambia mtandao huu muda mfupi uliopita kuwa kikosi chao kilitua jijini Dar es Salaam majira ya saa sita usiku na kesho kitaingia kambini kuinolea makali Coastal Union FC.

"Tumefurahishwa na namna timu inavyocheza na kupambana kupata ushindi, kesho itaingia kambini kujiandaa kwa mechi ya ligi kuu dhidi ya Coastal," amesema Dk Tiboroha.

Yanga SC iliyoshinda bao 1-0 dhidi ya mabingwa hao wa 1988 wa Tanzania Bara katika mechi ya mzunguko wa kwanza msimu huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Februari 4, mwaka huu, itaingia Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumatano ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union FC msimu uliopita kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video