Msemaji wa timu ya Ruvu Shootings Masau Bwire amelalamikia uamuzi mbovu michezo ya ligi kuu Tanzania bara hasa kuelekea katika hatua hii ya mwisho katika kinyang'anyiro hicho.
Bwire ametoa malalamiko hayo mara baada ya timu yake ya Ruvu Shooting kujikuta ikipoteza mchezo wao dhidi ya kagera Sugar kwa kufungwa mabao 2-1.
akifanyiwa mahojiano na kituo cha redio cha EFM, Bwire alisema kuwa imefikia hatua badala ya kucheza soka sasa linachezwa Sokomoko huku akiongeza kuwa goli la kwanza la Kagera Sugar lilikuwa ni dhahiri shahiri la kuotea lakini mwamuzi alijifanya kama haoni vile.
"Jambo la kushangaza mchezaji wetu aliingia katika eneo la hatari na kukwatuliwa na mabeki wawili wa Kagera Sugar lakini mwamuzi aliacha na kujifanya kama hajaona tena, wakati ukiangalia goli lao la kwanza lilikuwa ni la kuotea kabisa"
Lakini katika hatua nyingine, Masau Bwire aliliongelea suala la vyumba vya kubadilishia nguo, ambapo alionyesha kusikitishwa huku akisema kuwa endapo wachezaji wakiingia kwenye vyumbani hivyo kamwe hawataweza kurudi uwanjani vinginevyo wataumwa na matumbo ya kuharisha kutokana na hali na mazingira mabovu kabisa ya vyumba hivyo.
Timu kadhaa zimekuwa zikiadhibiwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kukata kuingia katika vyumba vya kubadilishia uwanjani hapo ikiwemo Yanga na kupigwa faini, katika hilo Masau Bwire amesisitiza kama suala la adhabu ya faini wapewe tu kuliko kuhatarisha afya za wachezaji wao


0 comments:
Post a Comment