Hii ndiyo ligi kubwa nadhani ulimwenguni kuliko ligi nyingine yeyote, si nyingine bali ni Ligi ya mabingwa ulaya.
Mechi Kali kwa usiku wa Leo ni hii ya mahasimu wa jadi, Madrid Derby.
Baada ya Madrid 'Derby' ya msimu ulioisha katika ligi hii hii ya mabingwa ulaya kumalizika kwa Real Madrid kuibuka kimasomaso kwa ushindi wa mabao 4-1 katika mtanange wa fainali, sasa wamekutana Tena katika robo fainali.
Kama takwimu (statistics) zinafanana hivi... Hebu cheki.
Msimu uliopita Atletico walikutana na Barcelona bila kukosea Mara 6, cha kushangaza Barcelona hakufanikiwa kushinda mechi hata moja.
Msimu uliopita Atletico walikutana na Barcelona bila kukosea Mara 6, cha kushangaza Barcelona hakufanikiwa kushinda mechi hata moja.
Na Barcelona walitolewa katika hatua kama hii wanayokutana na Atletico Madrid.
Msimu huu Atletico wamekutana na Real Madrid, na kama ilivyokuwa kwa Barcelona msimu uliopita vivyo hivyo Real Madrid hajashinda mechi hata moja kati ya 6 walizokutana msimu huu ..
Real Madrid katika ubora wao wa kutikisa nyavu pamoja na kuwa mbele ya Atletico hadi sasa katika msimamo wa ligi bahati mbaya zaidi anakutana na hasimu wake huyo ambaye hajaweza kumfunga hata mechi moja msimu huu.
Uzoefu kwa kiasi kikubwa huchangia katika matokeo ila kwa aina ya soka wanalolicheza hawa atletico basi sina shaka kuchelewa kulala na kamwe hakuna mtu atakayejuta katika hilo kutokana na ubora wa timu zote mbili.
Madrid akishinda basi ni kutokana na aina ya wachezaji alionao na pia uzoefu katika michuoano hiyo.
Ila akishinda Atletico ni kwa sababu aina ya uchezaji na muunganiko wa timu (Team chemistry) waliyo mayo na sio uzoefu katika michuano kikubwa.
Yeyote anaweza kuibuka mshindi ila gem ya Leo.


0 comments:
Post a Comment