Monday, April 6, 2015


SHIRIKISHO la kandanda Tanzania (TFF), limeiandikia barua Klabu ya Simba likiitaka kuhakikisha inakutana na nyota wa Yanga, na mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita, Mrundi, Amissi Tambwe kwa lengo la kumaliza tofauti zao.


Hatua hiyo imekuja kutokana na Tambwe kuishtaki Simba kwa madai ya kutolipwa haki yake ya kiasi cha dola za kimarekani, elfu 11 (11,0000), zaidi ya Sh milioni 20 za Kitanzania, kama fidia ya kukatishwa mkataba wake kabla hajasaini Yanga siku hiyohiyo baada ya kuachwa.


Katibu wa Simba, Stephene Ally, alikiri kupokea barua hiyo na kusema walikuwa wanamsubiri Tambwe arejee kutoka Zimbabwe alikokwenda na klabu yake kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kuchuana na FC Platinum.


 Tambwe aliifungia Simba magoli 19 mwaka jana

“Ni kweli tumepokea barua kutoka TFF kutuambia tukae chini na Tambwe ili tuelewane kuhusu madai yake. Tumelikubali hilo ila kwa sasa tunasubiri arudi kutoka Zimbabwe ili tuweze kuzungumza naye,” alisema Ally.

Simba imekuwa na rekodi mbaya ya kuvurugana na wachezaji wake kimaslahi, huku hivi sasa ikiwa na mvutano na nyota wake, Hassan Kessy.


Tayari TFF limetoa tahadhari kwa timu aina ya Simba, kwamba zinaweza kujikuta zikifungiwa usajili kutokana na kuwepo kwa kesi za madai ya malipo.


0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video