Sunday, April 26, 2015


Mbeya City Fc  imefanikiwa kuvuna pointi zingine tatu muhimu baada ya ‘kuidabisha’ Kagera Sugar kutoka Bukoba Mkoani Kagera bao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara  uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika mchezo huo ulioanza kwa taratibu huku kila timu ikijaribu kusoma mbinu za mwenzake, City ilikuwa ya kwanza kulifikia lango la Kagera Sugar  mnamo dakika ya 5 ambapo mpira ulioanzia katikati ya uwanja kwa Kenny Ally  ulimfikia Rafael Alfa  aliyetoa pasi nzuri kwa Fredy Cosmas lakini shuti la mshambuliaji huyo lilishindwa kulenga lango na mpira kutoka nje.
DSC_0197
Paul Nonga (26) akimpongeza Rafael Daud Alfa baada ya kufunga bao kwa mkwaju wa penalti.
Dakika 10 baadae Kagera Sugar walijibu mashambulizi  langoni mwa City lakini uimara wa golikipa Hannington Kalyesubula ulimnyima mshambuliaji Mandawa wa Kagera Sugar nafasi nzuri ya kufunga bao kwa timu yake.
Timu ziliendelea kushambuliana kwa zamu na wakati mchezo ukielekea mapumziko Fredy Cosmas alifanikiwa kuiwahi pasi ya Deus Kaseke akiwa ndani ya eneo la penalti  lakini wakati akijiandaa kufunga bao alifanyiwa  madhambi na mlinda mlango Kagera Sugar na mwamuzi kuamuru kupigwa mkwaju wa penalti.
Kiungo ‘fundi’  Rafael Alfa alifanikiwa kukwamisha wavuni mkwaju huo wa penalti na kuinadikia City bao la kuongoza kabla mwamuzi hajapuliza kipyenga kuashiria kumalizika kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza ambapo City ilikwenda kwenye vyumba vya kupumzikia ikiwa mbele kwa bao 1-0.
DSC_0183
Deus Kaseke (kushoto) akijindaa kumtoka mlinzi wa Kagera Sugar
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Juma Mwabusi katika kipindi cha pili kwa  kumtoa Fredy Cosmas, Mwegane Yeya na John Kabanda na nafasi zao kuchukuliwa na Peter Mapunda,Peter Mwalyanzi na Hamad Kibopile yaliiongeza nguvu City na hatimaye kufanikiwa kupachika bao la pili kupitia Deus Kaseke aliyeunganisha vyema mpira uliopigwa na Peter Mwalyanzi kutoka wingi ya kushoto.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha usingizini Kagera Sugar na kuanza kucheza mpira kwa kasi lakini juhudi zao ziliishia kwenye mikono ya golikipa Hanington Kalyesubula  au mipira yao kuokolewa na safu ya ulinzi ya City iliyokuwa chini ya nahodha Juma Nyosso ‘Coulibaly’.
DSC_0216
Peter Mwalyanzi (katikati) akiwatoka walinzi wa Kagera Sugar
Akiwa kwenye ‘ubora wake’ kiungo mshambuliaji Peter Mwalyanzi alindelea kuinyanyasa ngome ya Kagera Sugar ambapo dakika ya 85  nusura aipatie City bao la 3 baada ya kufanikiwa kuuwahi mpira aliotanguliziwa na Paul Nonga na kufanikiwa kumlamba chenga Salum Kanoni lakini shuti lake lilipaa juu kidogo ya lango la Kagera Sugar hivyo hadi dakika  90 zinakamilika City ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0.
Mara baada ya mchezo kocha Mwambusi aliwashukuru vijana wake kwa ‘kupambana’ na kufanikiwa kupata pointi tatu muhimu huku kuwaomba kujiweka tayari kwa mchezo unaofuata dhidi ya Tanzania Prison utakaochezwa jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Sokoine.
IMG_0348
Kocha Juma Mwambusi akizungumza na wana habari mara baada ya mchezo
“Tumecheza vizuri, nawashukuru kwa kupambana na hatimaye tumepata matokeo, hili ni jambo jema kwa sabbu tayari tumesogea nafasi nyingine kwenye msimamo wa ligi,naomba tujiweke tayari kwa mchezo ujao ambao pia ni muhimu zaidi, tunarudi kufanyia kazi mapungufu tuliyoyaona leo kwa sababu tumetengeneza nafasi nyingi lakini tumetumia chache,naamini kama tungekuwa makini tungeshinda goli nyingi zaidi” alisema Mwambusi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video