Thursday, April 23, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Okwi amekuwa nguzio mhimu katika mafanikio ya Simba msimu huu na anapokosekana uwanjani, timu hiyo imekuwa ikipata matokeo mabovu.'

UCHAWI, mchecheto au vimbwanga! Vyovyote unaweza kusema kutokana na kiungo mshambuliaji wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, jana kupewa tunguli na mmoja wa mashabiki wa klabu hiyo ya pili kwa ukongwe nchini.

Mara tu baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) waliyoshinda 4-0 dhidi ya maafande wa Mgambo Shooting Stars, Okwi alipewa tunguli na mmoja wa mashabiki wa klabu hiyo waliokuwa wamekaa juu ya lango kuu la ndani ya Uwanja wa Taifa.

Okwi alipokea tunguli hilo na kwenda nalo hadi ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo na alitoka nalo vyumbani huko na kuingia nalo kwenye basi lao kubwa walilopewa na wadhamini wa klabu hiyo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yao ya Kilimanjaro.

Mkali huyo wa mabao alionekana akicheka na kufurahia kwa kupewa zawadi hiyo ya tunguli ambayo huenda mtoaji aliamini itamwongezea 'uchawi' wa mabao Mganda hiyo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video