Beki na wakati mwingine kiungo wa Chelsea Kurt Zouma, amesema kuwa ana ndoto za siku moja kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or) katika kipindi chake atakachokuwa anacheza soka.
Zouma mwenye uraia wa Ufaransa mpaka sasa amecheza michezo 11 ya ligi, huku mara nyingine akicheza kama beki wa kati na wakati mwingine kama kiungo mkabaji.
Amekiri kuwa ana malengo makubwa sana na mchezo wa soka na kusistiza kuwa anataka kufuata nyayo za beki wa zamani wa Italia Fabio Cannavaro kwa kushinda tuzo hiyo akiwa kama beki, kitu ambacho kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ni ndoto kutokea.
"Ndiyo ni ndoto yangu hiyo,” Zouma aliliambia Canal.
Zouma amekuwa akifananishwa na mlinzi wa zamani na nahodha wa Chelsea Marcel Desailly kutokana na uchezaji wake na pia uwezo wake wa kumudu nafasi zaidi ya moja uwanjani
"Mara nyingi watu wamekuwa wakinifananisha na Marcel Desailly, ni kweli namkubali kwani alicheza kwa mafanikio makubwa sana,” aliongeza. “Desailly ni mtu mzito sana katika medani hii ya soka, amecheza michezo mingi sana, " Zouma alimalizia.

0 comments:
Post a Comment