Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kikosi chake kimejipanga vizuri katika michezo iliyobaki katika ligi kuu nchini Uingereza ili kujinyakulia ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.
Vinara hao wa ligi hiyo kali duniani,licha ya kuwa na mchezo mmoja mkononi lakini bado wapo kileleni kwa tofauti ya pointi 7 na wanaoshika nafasi ya pili Arsenal.
Chelsea inahitaji pointi 15 katika mechi 8 zilizobaki ili kuchukua kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2009/2010. "Huu ndio wakati muhimu sana,hapa ndio kila kitu kinaamuliwa,wanaoshuka daraja,wanaoenda klabu bingwa na anaechukua ubingwa " alisema Mourinho "Unaweza kufanya vizuri kwa miezi sita,saba,nane,tisa lakini wakati huu ukifika ndio wa umuhimu sana,sisi tumejiandaa vizuri katika kipindi hiki na tunahitaji ubingwa "aliongeza mreno huyo.
Chelsea itasafiri jumapili hii kwenda kucheza na Qpr kabla ya kurudi Stamford bridge kuikaribisha Manchester United na baadaye mwishoni mwa mwezi huu kucheza na Arsenal katika uwanja wa Emirates.


0 comments:
Post a Comment