Hali ya uwanja wa Kambarage jioni hii
MWISHONI mwa wiki iliyopita mechi ya Kagera Sugar dhidi ya Simba iliyotakiwa kupigwa uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga iliahirishwa kutokana na uwanja kujaa maji kutokanana mvua zinazoendelea kunyesha mpaka sasa mkoani humo.
Mechi hiyo ilichezwa jumatatu ya wiki hii na kushuhudia Simba wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Mabao ya Simba siku hiyo yalifungwa na Ramadhan Singano na Ibrahim Hajibu kwa mkwaju wa penalti,wakati Rashid Mandawa aliwafungia Kagera goli la kufutia machozi.
Kumbuka siku moja baadaye baada ya mechi ya Simba kuahirishwa (jumapili iliyopita) pambano la Stand United dhidi ya Mtibwa Sugar lilivunjika dakika ya 33' kutokana na mvua kubwa kunyesha na mechi hiyo ilichezwa jumatatu asubuhi.
Wakati mechi hiyo inavunjika Haruna Chanongo alikuwa amefunga goli dakika ya 12 na kesho yake wakatoka suluhu (0-0) katika dakika 57 zilizosalia, hivyo Stand kushinda 1-0.
Kagera Sugar wameandika rekodi nyingine leo baada ya pambano lao dhidi ya Ruvu Shooting kuahirishwa jioni hii kutokana na uwanja kujaa maji kutokana na mvua.
Hivyo mechi hiyo itachezwa jumatatu jioni.
kesho Stand United watacheza na Polisi Morogoro katika uwanja huo wa CCM Kambarage.


0 comments:
Post a Comment