Saturday, April 25, 2015

Na Mahamud Rajabu
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara AZAM FC, leo wameendelea vizuri na mawindo yao ya nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia kuishindilia Stand United mabao 4-0, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,jijini Dar es Salaam.
kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 45 baada ya kucheza michezo 23, ikiwa nyuma ya Yanga SC yenye pointi 52 za mechi 23 na mbele ya Simba SC yenye pointi 41huku ikiwa imecheza mechi 24.
Mabao ya Azam yaliwekwa kimiani na Gaudence Mwaikimba(2), Farid Malik na Mshambuliaji kutoka nchini Uganda Brian Majwega. Majwega alifunga dakika ya 14 akiunganisha kwa shuti maridadi krosi ya kiungo hodari Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Sure Boy tena akapiga krosi nzuri iliyounganishwa nyavuni na Mwaikimba kwa kichwa krosi dakika ya 37.
Mwaikimba tena, akaifungia Azam FC bao la tatu dakika ya 62 akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Stand, John Mwenda kufuatia krosi ya Sure Boy.
Farid Malik aliyetokea benchi kipindi cha pili, aliifungia Azam FC bao la nne dakika ya 89, akimalizia kazi nzuri ya Kipre Tchetche aliyetokea benchi pia.
Azam : Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Agrrey Morris, Serge Wawa, Mudathir Yahya/Bryson Raphael dk55, Frank Domayo, Salum Abubakar, Didier Kavumbagu/Kipre Tchetche dk67, Gaudence Mwaikimba/Farid Malik dk84 na Brian Majwega.
Standa United: John Mwenda, Revocatus Richard,  Abuu Ubwa/Yassin Mustafa dk, Jisend Mathias, Peter Mutabuzi, Jonh Nganga, Pastory Athanas/Salum Kamana dk73, Hamisi Shengo, Abasalim Chidiebele, Kheri Mohammed na Tola Anthony/Vitalis Mayanga dk46.

Katika mchezo mwingine uliopigwa katika dimba la sokoine jijini Mbeya, Timu ya soka ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera.
Mabao ya Mbeya City yalifungwa na Rafael Alfa Dakika ya 45 na Deus kaseke Dakika ya 55.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video