Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
LIGI Kuu Tanzania Bara itaendelea kesho kwa mechi tatu, huku maafande wa Ruvu Shooting wakipania kuishusha Simba katika nafasi ya nne.
Kikosi cha kocha mkuu Mkenya Tom Olaba cha Ruvu Shooting Stars kilichoibana kwa sare ya 1-1 Mbeya City FC mjini Mbeya mwishoni mwa wiki, kitashuka Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pawani kuwakaribisha Ndanda FC.
Masau Bwire, msemaji wa Ruvu Shooting Stars, amesema jijini hapa leo kuwa wamepania kuthibitisha kwamba hawakubahatisha kuifunga Ndanda FC mjini Mtwara mzunguko wa kwanza.
Amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanashinda mechi hiyo ili kuishusha Simba katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi ya Bara kwa kufikisha pointi 24 sawa na Kagera Sugar FC waliopo nafasi ya tatu.
"Tunahitaji ushindi katika mechi yetu ya kesho ili kuthibitisha kwamba sisi (Ruvu Shooting Stars ni timu bora. Kumbuka tuliwafunga Ndanda FC mabao 3-1 kwao mjini Mtwara na kumfukuzisha kazin aliyekuwa kocha mkuu wao (Dennis Kitambi). Tumejiandaa kuhakikisha tunawapiga tena kesho," ametamba Masau.
Ndanda FC iliyopo nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19, itaingia Uwanja wa Mabatini kesho ikisaka heshima ya kutopoteza mechi ya sita mfululizo tangu walipofungwa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Simba SC Januari 17.
Katika mechi hiyo, Ruvu Shooting Stars yenye pointi 21 katika nafasi ya tisa, inamkosa beki wake wa kati George Michael ambaye kesho atamaliza adhabu ya kufungiwa mechi tatu za VPL na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupatikana na hatia ya kumkaba koo mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita, Mrundi Amisi Tambwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Januari 18.
Mtibwa vs Polisi Moro hapatoshi Manungu
Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, mabingwa wa Tanzania Bara 1999 na 2000, Mtibwa Sugar FC watakuwa na kibarua kigumu mbele ya majirani zao Polisi Morogoro FC kesho.
Mtibwa Sugar FC inayonolewa na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime, haijapata ushindi katika Ligi Kuu Tanzania Bara tangu Oktoba 26, mwaka jana ilipoifunga Mbeya City FC mabao 2-0 jijini Mbeya na kikosi hicho cha wakatamiwa wa Manungu, hakina rekodi nzuri katika mechi zake dhidi ya kikosi cha Adolf Richard cha Polisi Morogoro FC.
Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Oktoba 18, mwaka jana. Mara nyingi mechi za Polisi Morogoro FC dhidi ya Mtibwa Sugar FC humalizika kwa sare.
JKT Ruvu vs Tanzania Prisons vita nyingine Chamazi
Kikosi cha Tanzania Prisons kilichopigwa 'mkono' (mabao 5-0) dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumamosi, kitashuka Uwanja wa Azam jijini kuwakabiri wenyeji JKT Ruvu kesho jioni.
Kikosi cha JKT Ruvu kinachonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Felix Minziro, kinahitaji ushindi kesho ili kizishushe timu za Coastal Union FC, Ruvu Shooting Stars, Stand United FC na Mtibwa Sugar FC zinazokamata nafasi za 5-8 katika msimamo wa ligi ya Bara kwa sasa.
Kocha mkuu wa Tanzania Prisons ambaye inadaiwa kuwa amekalia kuti kavu kutokana na timu yake kukaa mkiani kwa muda mrefu, ataingia Uwanja wa Azam akisaka heshima ya kutopoteza mechi uwanja huo msimu huu baada ya kuwalazimisha suluhu mabingwa watetezi Azam FC katika mechi iliyopita baina ya timu hizo.
Safu ya ushambuliaji ya JKT Ruvu inayoongozwa na Samwel Kamuntu, ina nafasi ya kuitungua mabao mengi tena Prisons ambayo inamkosa beki wake mahiri wa kati, Nurdin Chona ambaye alitolewa kwa kadi ya pili ya njano katika mechi iliyopita dhidi ya Simba SC Jumamosi.

0 comments:
Post a Comment