Monday, March 30, 2015

Fainali za soka za kombe la Dunia mwaka 1990 zilizochezwa Italia zitabaki kuwa michuano pekee yenye kumbukumbu nzuri na bora kwa Afrika si kwa sababu ilifanikiwa kufika robo fainali, bali ni kwa namna ambavyo wana wa bara hili walivyokuwa wanalisakata gozi.
Ikumbukwe kwenye fainali hizo Misri na Cameroon ndiyo pekee ziliwakilisha bara hili, ambapo mafarao waliambulia patupu kwa kutolewa mapema na hatimaye kuwaacha ‘Simba wasioshindika’ wakilipigania bara letu ughaibuni.
Mashabiki wa soka zaidi 73,780 waliojazana San Siro wengi wao wakiwa na kiu ya kumshuhudia Diego Maradona walipigwa na butwaa baada ya dakika 90 kumalizika Cameroon ikinyamazisha Argentina bao 1-0 lilowekwa kimiani na Francois Omam-Biyik akiunganisha krosi ya mtaalamu, Cyrille Makanaky, kwenye dakika ya 67.

DSC_0053
Hassan Mwasapili (mwenye mpira).
Hapo ndipo ninapoikumbuka soka safi waliyoionyesha vijana wa Cameroon tangu waliposhinda gemu hiyo hadi wanatolewa ‘kimizengwe’ na England kwenye hatua ya robo  fainali, licha ya kucheza vizuri kama timu uwezo wa mchezaji mmoja mmoja uwanjani hakika ilikuwa burudani tosha kwa mashabiki wa soka.
Licha ya kikosi chote kucheza vizuri lakini kwenye kinyang’anyiro hicho huwezi kuacha kuwataja nyota walikuwa wanacheza safu ya ulinzi hasa wa pembeni ambako mara zote alikuwa akisimama Benjamin Masssing, kulia na Bertin Ebwelle, kushoto.

ebwelle
Ebwelle ni mmoja wa mabeki bora wa kushoto kuwahi kutokea kwenye soka la Afrika licha ya kutokutajwa sana , akiwa kwenye ubora wake aliweza kuwadhibiti wakali wa Argentina Abel Balbo, Diego Maradona na Claudio Caniggia ambao waliokuwa wanajaribu kupita upande wake kwenye mchezo huo wa kwanza dhidi ya Argentina.
Hapa kwetu Bongo unapoanza kuzungumza juu ya nyota waliotamba kwenye nafasi hizo huwezi kuacha kuyataja majina kama,Yassin Abou Napil,Kenny Mkapa, Rafae Paul, Twaha Hamidu ‘Noriega’,Samli Ayoub, Alfonce Modest, Mecky Mexime,Said Sued,Shadrack Nsajingwa,Amir Maftah,Kasim Issa na wengine wengi ambao walitamba kipindi chao lakini hawakupata kuandikwa sana.

DSC_0090
Vivyo hivo kwenye soka la kizazi cha sasa hapa nchini kwenye nafasi hizo huwezi kuacha kuwataja nyota kama Juma Jabu, James Luhende , Hasani Kessy, Nassor Masoud,Juma Abdul,Abdul Ntiro, Mohamed Tshabalala na wengine wengi kundi ambalo huwezi kuacha kumjumuisha nahodha wa Mbeya City Fc ya Mbeya Hassan Mwasapili.
Hakika Mwasapili ni moja kati ya mabeki bora wanaocheza soka la kisasa akitumika kama mchezaji anayeshambulia na kuzuia bila kujali anacheza upande upi wa ulinzi iwe kulia ama kushoto ambako mara nyingi huwa nacheza.
Ukitizama orodha ya nyota wa zamani waliowataja hapo hakika wengi walikuwa na vipaji lakini ule uwezo wa kucheza vizuri fullback zote mbili yaani kulia na kushoto walikuwa nayo wachache, ni wazi huwezi kumpanga Oscar Joshua acheze kulia ukategemea utafanikiwa.

DSC_0408
Baada ya kupita Fredy Felix Minziro na kuibuka Lawrence Mwalusako na baadae Kenny Mkapa na wachache baadhi katikati kulishuhuudia wa nyota wenye uwezo huo wa kucheza kulia na kushoto kama mabeki licha ya wao kwa maana ya kutumia mguu wa kushoto.
Hivyo ndivyo unavyoweza kuanza kumzungumzia Hassani Mwasapili, nahodha wa City ambaye amekuwa kwenye kiwango bora ndani ya kikosi kwa misimu miwili sasa tangu timu hiyo ya Mbeya alipopanda na kuonyesha makali yake kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara.

DSC_0033
Kwa wanaomjua au wanaofika viwanjani kuona michezo ya City ni wazi watakubaliana kuwa Mwasapili ni aina ya mabeki ambao wamewatajwa hapo juu kwa maana kuwa wanakuwa na uwezo lakini si wale wanaoandikwa ama kutajwa sana kwenye vyombo vya habari.
Pengine hapo ndipo kunapoibua maswali kwa wadau wengi kuwa huenda kutokuitwa kwake timu ya Taifa kunasababishwa na hali hiyo? au wanaoteua wachezaji wa Taifa Stars bado wamekariri kuwa ni lazima utoke Simba na Yanga ili kucheza Stars………..
ITAENDELEA JUMATATU IJAYO

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video