Na Oswald Ngonyani
Jina lake linaonekana kuzungumzwa tena na tena kwa sasa, hii inatokana na mwenendo usiotia matumaini kwa kikosi anachokinoa, mwenendo ambao tayari umekwisha wagawa mashabiki wengi wa ‘The Gunners’.
Kitendo cha kuendelea kuwa mdebwedo kwa Man United ni miongoni mwa sababu ambazo zimewafanya mashabiki wengi wa Arsenal kumuona Arsene Wenger kama sababu ya timu yao kuasua sua.
Wengi wanaamini kuwa Wenger ana kikosi kizuri, tena kizuri sana tatizo linakuja katika namna ya kuwatumia wachezaji aliokuwa nao yaani mfumo wa kiuchezeshwaji ndani ya dimba lakini pia uteuzi anaoufanya kwa kikosi chake cha kwanza, wengi huamini kuwa anakosea.
Tangu ajiunge na Arsenal, Wenger amepitia katika nyakati tofauti tofauti, nyakati ambazo kwa kiasi fulani zimempa heshima kubwa sana lakini pia kwa upande mwingine zimemweka katika masononeko makubwa baada ya kukinzana na matakwa ya mashabiki wa timu husika.

0 comments:
Post a Comment