Winga wa klabu ya Liverpool Lazar Markovic sasa amefungiwa mechi nne baada ya kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu alipopewa kadi nyekundu katika mchezo uliopita wa kombe la klabu Bingwa Barani Ulaya dhidi ya klabu ya Fc Basel mwezi Disemba, ambapo mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kutoa sare ya kufungana mabao moja kwa moja.
Markovic mwenye umri wa miaka Ishirini, aliingia uwanjani akitokea benchi kipindi cha pili katika mtanange huo, lakini alijikuta akizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji Behrang Safari wa Fc Basel.
Akizungumza baada ya mchezo kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers, alisema akubaliani na maamuzi yaliyotolewa na Refa aliyekuwa anachezesha mchezo huo, na kusema yalikuwa maamuzi mabovu na kusisitiza kuwa Markovic akustahili kupewa kadi nyekundu.
"Kwa kweli ni uamuzi ambao haukustaili kabisa kutolewa kwa mchezaji wetu licha ya kufanya kosa kwani katika mchezo wa mpira wa miguu makosa kama hayo huwa yanatokea na wachezaji wamekuwa hawapewi adhabu kama hii ambayo inamdidimiza mchezaji kisoka," alisema Rodgers.
Kadi hiyo ya Markovic inamaanisha sasa mchezaji huyo ataikosa michezo inayofuata katika kombe la Uropa ambapo Liverpool ilishushwa kushiriki katika michuano hiyo baada ya sare waliyoipata.






0 comments:
Post a Comment