“Tumepokea kwa masikitiko matokeo haya, mpira wa
miguu unaumiza sana. Tulicheza kwa nguvu zote, tulikuwa na nia ya kushinda,
bahati haijawa upande wetu”.
“Tumepata nafasi nyingi na kupoteza, wenzetu
wametumia nafasi yao. Stand ni wazuri, kila timu sasa hivi inahitaji ushindi,
tunajipanga kwa mechi zijazo”
“Niwaomba mashabiki wa Simba wasiwe na ‘presha’
mpira ndivyo ulivyo. Tukubali matokeo, tujiandae kwa mechi ijayo”.
Haya yalikuwa maneno ya nahodha wa Simba, Hassan Suleiman
Isihaka baada ya mechi ya jana kumalizika kwa Mnyama kuchapwa bao 1-0 dhidi ya
Stand United uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment