Atarudishwa nyuma zaidi? Paul Scholes anaamini Wayne Rooney anaweza kucheza nafasi ya kiungo dhidi ya Uswizi jumatatu
NAHODHA wa England, Wayne Rooney anatakiwa kurudishwa katika majukumu ya kiungo katika mchezo wa jumatatu kuwania kufuzu fainali za Euro 2016 dhidi ya Uswizi, kwa mujibu wa Paul Scholes.
Simba Watatu walihangaika kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Norway katika mechi ya kirafiki jumatano ya wiki hii ambapo Rooney alifunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa penalti.
Lakini Scholes ambaye alishinda mechi 66 kwa Taifa lake, anaamini Roy Hodgson anaweza kumtumia nahodha wake nyuma zaidi watakaposhuka katika dimba la St Jakob Park mjini Basle.
Mzee wa maoni: Scholes anadhani Rooney ndiye mkali wa kupiga pasi katika kikosi cha Roy Hodgson kwa sasa
Nyota huyu wa zamani wa Manchester United anadai kuwa England imekosa kiungo mwenye uwezo kwa kupiga pasi za kwenda mbele baada ya kustaafu wa Steven Gerrard, lakini anaona Rooney anaweza kusaidia kuziba pengo hilo dhidi ya Uswizi.

0 comments:
Post a Comment