
Jembe la kazi: Ronaldinho amekubali mkataba wa miaka miwili kuicheza klabu ya Mexico ya Queretaro
KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Brazil na Barcelona, Ronaldinho ambaye ni mchezaji bora wa dunia mara mbili, amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Queretaro.
Nyota huyo mwenye miaka 34 ambaye aliwahi kuzichezea Paris St Germain na AC Milan, alikuwa mchezaji huru mwezi julai mwaka huu baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Brazil Atletico Mineiro.
"Tumefarijika sana kuongeza kiwango chetu leo (jana), tumempata mchezaji mwenye uzoefu mkubwa wa soka la kimataifa. Mshindi wa kombe la dunia 2002, mchezaji bora wa dunia mwaka 2004 na 2005" alisema taarifa ya klabu hiyo.

Makubaliano: Gwiji wa Brazil aliondoka Atletico Mineiro kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba
0 comments:
Post a Comment