Thursday, September 11, 2014

 
USAJILI wa Mbuyu Twite umeingia dosari baada ya klabu yake ya zamani ya FC Lupopo  ya Congo kuibuka na kusema bado ni mchezaji wake.

Katibu mkuu wa Lupopo, Consntatine Kapika yupo jijini Dar es salaam kudai fedha zao na wameshangazwa sana na kitendo cha Twite kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Yanga baada ya mkataba wa mkopo wa miaka miwili kumalizika.

Kiongozi huyo alisema viongozi wa Yanga walitakiwa kuwasiliana na Lupopo kama bado wanamhitaji Twite.

Kapika anajaribu kuwasiliana na viongozi wa Yanga akiwemo Ahmed Seif ‘Magari’, Abdallah Binkleb na katibu mkuu Beno Njovu, lakini wanamzungusha bila kupewa nafasi ya kuonana na viongozi wa juu wa Yanga.

Kapika alisema kama Yanga watashindwa kukaa meza moja na Lupopo, basi nyaraka zote kuhusu mkataba wa mchezaji huyo zitapelekwa TFF, CAF na hatimaye FIFA.

Taarifa kamili tunaifuatilia kwa kina kutoka pande zote mbili, Yanga na Lupopo.



0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video