
Kwenye rada: Tottenham wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili Mateo Musacchio.
Imechapishwa Agosti 4, 2014, saa 2:48 asubuhi
WATUKUTU wa London, Tottenham wanaendelea na mazungumzo na klabu ya Villarreal ili wamsajili beki Mateo Musacchio kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 20.
Beki huyo imara wa Argentina amekuwa akizivutia klabu nyingi miaka ya karibuni.
Sio mrefu zaidi, lakini amekuwa akicheza vizuri na kukaba kwa 'staili' ya nahodha zamani wa Argentina, Daniel Passarella.
Anafahamika sana na kocha Spurs Maurico Pochettino ambaye anatafuta beki atakayeimarisha safu yake ya ulinzi na yupo tayari kusikiliza ofa juu ya beki wake Michael Dawson.
Wakati huo huo kuna wasiwasi kama Younes Kaboul ataendelea kubakia klabuni hapo.
Japokuwa hakuna uthibitisho wa kiofisi juu ya dili hilo, kocha wa Villarreal, Marcelino alisema: 'Ni jambo la sehemu tatu: mchezaji, mnunuaji na klabu.
'Kama ninavyosema mara kwa mara, kama klabu inamuuza mchezaji muhimu ni kwasababu masharti yamefikiwa.
'Haitakuwa rahisi kumpata mbadala, lakini suluhusisho litapatikana.'

Yupo sokoni: Maurico Pochettino anaendelea kujiimarisha kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
0 comments:
Post a Comment