
HATIMAYE
Manchester United imeingia katika hatihati kwa kumsajili beki wa Sporting
Lisbon, Marcos Rojo, ingawa njia zilizotumika ni za uhamisho wa kisasa.
Kitendo
cha United kuzungumza na mchezaji huyo wiki iliyopita kulisababisha mgongano baina
ya Sporting na Kundi la Uwekezaji la Doyen Sports (walioshughulikia uhamisho wa
Radamel Falcao kwenda Monaco na linamjumuisha mkurugenzi mkuu wa zamani wa Chelsea,
Peter Kenyon na wakala mwenye nguvu kubwa, Jorge Mendes).
Doyen
wanadai kuwa wanamiliki 75% ya haki za
kiuchumi za Rojo, na wameripotiwa kutaka kukata asilimia ya ada iliyolipwa na United,
lakini suala hilo limekataliwa. United wamepitia rekodi na kusema suala hilo
lina utata mkubwa.
Siku
ya jumanne, Sporting walitangaza kupitia soka la hisa kuwa wamemuuza Rojo kwa
dau la Euro milioni 20 (paundi milioni 16) na kusema kuwa watailipa Doyen fedha
za uwekezaji wa awali ambazo ni milioni 3 (paundi milioni 2.4), lakini waligoma
kutoa zaidi ya hapo.
Bado
utata umeendelea kuwepo na hapo ndipo wamiliki wa kampuni ya ‘Third-party’ (TOP)
inayohusika na masuala ya wuchezaji inaibua maswali ambayo hayana majibu kuhusu
fedha, uchumi na usimamizi wa mauzo ya wachezaji..
Doyen
kama wafadhili wa mpira wa miguu walieleza kuwa hawahusiki na kuwasimamia
wachezaji au kusimamia uhamisho wao. “Hatumiliki wachezaji. Tunajihusisha benki
ya Barclays au benki nyingine wakopeshaiji wa mikopo, lakini hatuwezi kudhibiti
maisha au mshahara wa mchezaji. Sisi Kamwe hatufanyi chochote kinyume na matakwa
yao”, alisema Mkurugenzi mtendaji, Nelio Friere alipoulizwa maswali juu ya TOP
mwaka uliopita.
Third-party
wanahusika na uwekezaji wa nje na kufikia makubaliano na klabu juu ya ada ya
uhamisho na kuzitunza haki za kiuchumi za mchezaji anapouzwa.
Kuna
makundi ya uwekezaji yaliyoanzishwa mahususi kwa masuala haya; moja wapo ni
Doyen Sports ambao wamewekeza paundi milioni 80 kwa ajili ya kutunza vipaji vya
wanamichezo duniani. (Kikosi walichotengeneza ni mchezaji wa Olympiakos,
Alberto Botia na Manu del Moral wa Sevilla). Pia mchezaji wa kimataifa wa Hispania
Alvaro Negredo, Falcao wa Monaco na mchezaji wa karibuni ambaye amesajiliwa na
Manchester City, Eliaquim Mangala) nao walihusishwa na kampuni hii.
Kiukweli
dili la kumchukua beki huyu wa zamani wa Porto, Mangala kwenda England halikuwa
rahisi kwasababu halikuhusisha tu klabu bali Doyen nao walihusika. Kila mtu
alitaka kupata chake katika ada ya uhamisho.
Akiwasili: Marcos Rojo alitua nchini England jana kukamilisha taratibu za usajili katika klabu ya Man United.
Uhamisho
wa Falcao kutoka Porto kwenda Atletico Madrid mwaka 2011, Doyen Sports na Atletico
waligawana ada ya uhamisho ambapo kila upande ulichukua 50%.
Hata
alipouzwa katika klabu ya Monaco kwa Euro milioni 60, Atletico waligawana fedha
iliyopatikana na wawekezaji hao.
Kwasasa
kampuni ya TPO imepigwa marufuku nchini England, Ufaransa na Poland. Lakini
katika maeneo mengine bado inaendelea kuwepo hususani Hispania, Ureno, Ulaya
mashariki na Amerika kusini, hasa Brazil.
Kwa
mujibu wa ripoti ya kampuni ya uhasibu ya KPMG, TOP kwa 27% na 36% wanamiliki wachezaji
katika soko la usajili nchini Ureno, na
sasa namba imeongezeka na kufikia 40% kwa ligi za Ulaya mashariki.
Wakati
kwa Hispania takwimu zinaonesha kuwa TOP wanahusika kwa 8%, na katika misimu ya
karibuni, takwimu zimeongezeka kwa klabu za La Liga.
Nchini
Brazil, 90% ya wachezaji wake wanaocheza ligi kuu, haki za kiuchumi zinamilikiwa
na wawekezaji. Inafahamika kuwa suala hili limeleta faida na hasara.
UEFA
na Rais wake Michel Platini hawawezi kulipuuza suala hili. Katika mkutano wa
mwaka wa FIFA uliofanyika mwezi septemba mwaka jana alimuomba Rais wa FIFA, Sepp
Blatter kutengeneza sheria ya kuwazuia TOP, akisema kuwa, “Tatizo la wachezaji
kumilikiwa na makumpuni yenye misingi ya kodi na mawakala wasiofahamika.
“Rahisi
tu, baadhi ya wachezaji hawana uhuru katika masuala yao ya kisoka na wanauzwa
kila mwaka ili watu wasiojulikana wavune mapato na kujipatia hela kutoka kwenye
masuala ya mpira”.
Platini
alitishia kwamba, kama FIFA na Blatter hawataweka sheria, UEFA italazimika
kutengeneza sheria yake ili kukabiliana na vitendo hivi ambavyo anahisi ni ‘Hatari
katika michezo’. Walipoulizwa juu ya madai ya Platini, Doyen Sport waligoma
kuzungumza chochote.

Chama
kinachosimamia wachezaji wa kimataifa cha FIFA, Fifpro Kiliweka wazi na kuunga
mkono kauli ya Platini. Mkurugenzi wa mawasiliano Andrew Orsatti alisema kuwa
chama hicho kinapingana na TOP kwa namba yoyote ile kwasababu kinakwenda
kinyume na haki za wachezaji kama binadamu na wafanyakazi.
Inawezekana
lengo la wawekezaji ni zuri, lakini ukweli ni kwamba uhusiano wa asiyenacho na
mwenye nacho unazidi kuongezeka katika soka. Matajiri wakubwa wameingia katika
soka kama vile Manchester City, Chelsea na Paris Saint-Germain ambao mamiliki wanamwanga
fedha za kutosha katika soka la wachezaji na mishahara.
Miamba
ya soka kama Manchester United na Barcelona imeongeza wigo wa mapato yake tangu
mwaka 2010; Barca aliongeza kwa paundi milioni 48 kati ya 2012-13 na 2013-14,
wakati Manchester United waliongeza paundi milioni 752 kwenye mkataba wa Adidas
(unaoanza mwaka 2015).
Klabu
kubwa zinaweza kujiendesha zenyewe, lakini fedha wanazopewa wanatakiwa
kuzitumia katika misingi ya sheria ya matumizi ya fedha. Pesa inahitajika
katika mpira na hapo ndipo TPO wanakuja.
Kitu
cha kuvutia ni kwa klabu kama Atletico Madrid, Benfica na Porto ambazo hutumia
TOP kwa kugawana hasara.
Ripoti ya KPMG ilisema asilimia inayomilikiwa na
Third-party haizidi asilimia 50, ni kati ya 10% na 40% ambayo inakubalika
(lakini suala la Rojo limekuwa tofauti), kwa maana ya wamiliki wa nje ndio wana
hisa kubwa zaidi katika maisha ya mchezaji huyo.
Javier
Tebas, Rais wa chama cha soka la Hispania aliruhusu uwekezaji wa fedha katika
soka kwa madai kuwa zitasaidia kuimarisha ushindani wa klabu za nchi hiyo.
Kutokana
na maamuzi hayo, TPO ndio chaguo kwa klabu nyingi za nchi hiyo. Kwahiyo maombi
ya Platini kupiga marufuku makampuni haya kama vile litashindikana, anaamini
mwanasheria wa michezo wa FIFA, Alumni Luis Villas Boas Pires.
“Sidhani
kama FIFA watapiga marufuku TOP,” aliuambia mtandao Goal.
“Kama
Uefa wataamua kupiga marufuku TOP, maamuzi kama hayo yatachukuliwa dhidi ya
sheria ya matumizi ya fedha ya Uefa”.
Lakini
ukweli ni kwamba, hata kama TPO watapigwa marufuku au la, bado kuna utata
mkubwa ambapo wawekezaji wanakuwa na nguvu zaidi juu ya wachezaji.
Kuna
haja ya kuchambua vizuri wawekezaji hao hata kama hawatapigwa marufuku kama ilivyo
kwa Ligi kuu Engalnd, lakini kamati ya utawala ya FIFA lazima ipewe nguvu ya
kuweka sheria nzuri ya kudhibiti TPO ili kuokoa mpira wa miguu.
Mkurugenzi
wa LFP, Tenas anaamini kuwa “sheria ya kuwasimamia ni TPO ni muhimu ikawekwa
ili kulinda haki”.
Villas-Boas
anaamini sheria ni muhimu kuanzishwa kwa lengo la kuzisaidia klabu juu ya suala
hili, lakini kuwapiga marufuku moja kwa moja halitakuwa jambo jema.
Aliongeza:
“Kupiga marufuku TPO hakutazuia wawekezaji kunua haki za kiuchumi za wachezaji-
watatafuta ujanja juu ya katazo hilo.Kama Sheria nzuri, usimamizi mzuri juuya wamiliki
wa haki za wachezaji itawekwa wazi, kutaifanya Uefa ipunguze wasiwasi wa athari
hasi za TPO”.
Kama ilivyo katika sheria ya matumizi ya
fedha, kuna haja ya kuanzisha utaratibu mzuri. Mwanasheria wa michezo, Daniel
Geey anasema njia pekee ya kupambana na TPO ni kutengeneza sheria inayowalazimu
kuweka mambo yote hadharani.
“Kudhibiti
TPO ni jambo gumu sana kutokana na utata uliopo juu ya mgongano wa kimasilahi,”
aliueleza mtandao wa Goal.
Jambo
la muhimu ni kwamba-TPO hawawezi kuzuiliwa, ukiangalia hali halisi ya klabu ya
Valencia. Mjadala wa mgongano wa masilahi umeibuka ambapo mmiliki wake, Peter
Lim alipewa mfuko wa uwekezaji ambao unahusisha wachezaji wawili waliosajiliwa
majira ya kiangazi-Rodrigo Moreno na Andre Gomes.
Hali
ya vikundi vya uwekezaji kujihusisha zaidi na masuala ya klabu, ni tishio
katika michezo. Kwa maana hiyo kuna umuhimu wa kuanzishwa kwa sheria ya
usimamizi wa TPO.
Hata
hivyo, Fifpro na Orsatti ndio wenye mamlaka au uwezo kwa kushughulikia utata
kama huu.
Wakati
Uefa na FIFA wakifikiria cha kufanya baadaye, Doyen Sports mwezi Aprili
walitangaza kutengeneza mkatati mpya wa pili ‘Doyen Sports II’-ambapo
watawekeza zaidi katika michezo wakianza
na paundi milioni 160 kwa ajili ya kusajili wachezaji wapya wenye vipaji
duniani.
Doyen
wanakuja na mpango huu ambao unasemekana kupunguza uovu ili kukwepa kupigwa
marufuku kimataifa. Hawataki suala la Rojo kutokea miaka ijayo.
0 comments:
Post a Comment