
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Imechapishwa Agosti 8, 2014, saa 4:00 usiku
Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara timu ya kandanda
ya Azam FC imeanza michuano ya Kagame Cup kwa suluhu ya kutofungana dhidi ya
moja ya timu tatu wenyeji wa michuano ya 40 ya Kagame Cup, timu ya Rayon Sports
. Mchezo huo wa kundi la kwanza ndio pekee ambao hakutoa goli/magali kati ya
michezo mitatu ya kwanza siku ya ufunguzi katika uwanja wa Amahoro, Kigali,
Rwanda.
Mchezo wa kwanza
wa kundi A ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 kati ya KMKM ya
Zanzibar na Atlabara ya Sudan Kusini. Mchezo wa pili ulikuwa ni ule kati ya
KCCA ya Uganda iliyoichapa Gor Mahia ya Kenya kwa mabao 2-1.
Mchezo wa Rayon na Azam ulikuwa na kasi, huku timu
hizo zikicheza kwa mpangilio kuanzia idara ya ulinzi hadi ya kiungo huku safu
zote za ushambuliaji zikikosa umakini
licha ya nafasi nyingi kutengenezwa. Ulikuwa ni mchezo wa kusisimua ambao
wachezaji wa pande zote walicheza kwa nguvu na kutimiza maagizo muhimu ya
walimu wao.
Mambo haya matatu nimeyaona kwa upande wa Azam FC
na kwa kiasi kikubwa yamechangia matokeo hayo ambayo yanawafanya kuwa na pointi
moja moja kwa kila timu katika kundi A.
SALUM ABUBAKARY ALIPOTEZA NAFASI BORA ZAIDI
Salum Abubakary ni mchezesha timu
mzuri. Aliweza kutawala muda mwingi wa mchezo dhidi ya Rayon Sports lakini
mchezaji huyo wa kiungo alipoteza nafasi ya wazi pale alipo ' place' pembeni ya
lango na kuinyima timu yake bao katika dakika ya 48. Mshambulizi, Kipre Tcheche
alikimbia na mpira pembeni ya uwanja upande wa kushoto na kuingia nao katika
eneo la hatari na kupiga pasi nzuri ya mwisho kwa Salum ambaye alitokea
katikati ya uwanja. Ndani ya hatua sita kiungo huyo alipiga pasi pembeni ya
nyavu badala ya kupiga mpira golini akiwa hatua umbali wa hatua zisizozidi sita.
Nini alichotakiwa kufanya Salum?. Alitakiwa
kujibadilisha kutoka sifa za kiungo na kuwa mfungaji. Licha ya hivyo alipoteza
umakini na kupiga mpira akiwa amejiamini baada ya kuwa ' huru'. Alifanya kazi
nzuri katikati ya uwanja kwa kugawa pasi lakini kitendo cha kupoteza nafasi ya
wazi kimechangia matokeo ya sare kwa timu yake.
MBINU ZA KUSAKA MABAO, UMAKINI MDOGO KATIKA
UFUNGAJI
Kipre Tcheche alichezewa faulo karibu na maeneo ya
hatari na mlinzi wa Rayon Sports katika dakika ya 57. Akapoteza nafasi ya wazi
katika dakika ya 64 akiwa karibu na lango akaunganisha bila uelekeo mzuri mpira
wa krosi uliotoka wingi ya kulia na kuinyima timu yake nafasi ya kupata bao la
kuongoza katika mchezo huo uliokuwa mgumu na mkali muda wote. Safu ya
ushambuliaji ya Azam FC ilishindwa kujiamini na kufanya timu yao kupata sare ya
bila kufungana.
Didier Kavumbagu aliingia mahali kwa Hamis Mcha ‘
Vialli’ katika dakika ya 70, na kufanya safu ya mashambulizi kuwa na
washambuliaji watatu. Kipre, nahodha, John Bocco na Kavu. Azam ilitengeneza
nafasi za kutosha katika mchezo huo, na Kavumbagu alitengeneza nafasi nzuri kwa
Bocco katika dakika ya 80 lakini mshambulizi huyo wa timu ya Taifa Stars,
alipiga mpira huo juu akiwa hatua chache karibu na goli. Hizi ni baadhi tu ya
nafasi ambazo Azam walizipoteza na kuonyesha tatizo la umakini wakiwa katika
eneo la hatari la timu pinzani.
KUHIMILI MASHAMBULIZI
Mwadini Ally alionekana kufanya makosa katika
kipindi cha kwanza baada ya kutema mipira mingi, lakini alipojenga hali ya
kujiamini alikuwa mchezaji wa aina yake katika mchezo huo. Alimnyima bao mshambulizi hatari wa Rayon
Sports, Yossa Betram katika dakika ya 75 wakati mshambuliaji huyo alipojaribu
kufunga kwa mpira wa kichwa cha kushtukiza akiunganisha mpira wa krosi kutoka
upande wa kushoto wa Azam FC
Walinzi, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Aggrey
Morris na David Mwantika walicheza soka la kazi muda wote japo walitumia robo
saa ya mwisho ya mchezo huo kupokea mashambulizi kutoka kwa wenyeji ambao walipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki
wengi waliojitokeza kushuhudia mchezo huo. Azam walicheza kwa uvumilivu
japokuwa walionekana kuchoka kutokana na kucheza muda mwingi kwa lengo la
kupata bao ambalo lilikuwa karibu kupatikana. Matokeo ya sare si haki kwa
upande wao kwa sababu walitengeneza nafasi nyingi lakini hazikutumiwa vizuri,
lakini matokeo hayo kwa upande mwingine yana afadhali kwa sababu waliyasotea
kuyapata.
0714 08 43 08
Chanzo:shaffihdauda.com

0 comments:
Post a Comment