
Imechapishwa Agosti 2, 2014, saa 3:07 usiku
MALAWI wamefuzu hatua ya makundi ya kuwania tiketi
ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON 2015 nchini Morocco baada ya kuifunga
Benin kwa mikwaju 4-3 ya penalti.
Mechi iliyopita mjini Cotonou, Malawi walifungwa
bao 1-0 na leo wakiwa nyumbani wamepata ushindi wa aina hiyo, hivyo sheria ya
mikwaju ya penalti kutumika kuamua mshindi.
Bao pekee la ushindi kwa Malawi liligungwa na John
Banda katika dakika ya 13.
Malawi
ambao wapo nafasi ya 16 kwa nchi za Afrika katika viwango vya FIFA walitawala
mchezo kwa muda mrefu, lakini walishindwa kupata mabao mpaka penalti zikaamua.


Benin ndio walikuwa wa kwanza kulishambulia lango
la Malawi, lakini nyota wake Stephane Sessegnon alikosa nafasi kadhaa na kuipa
Malawi kupata faida ya ushindi kwa penalti.
Baada ya ushindi huo, Malawi watakabiliana na nchi
za Mali, Ethiopia na Algeria kwenye kundi B.
Wakati huo huo, Rwanda nao wamefuzu hatua ya
makundi kwa mikwaju ya penalti baada ya kufuta kipigo cha mabao 2-0 walichopata
ugenini dhidi ya Congo-Brazzavile.
Mabao mawili ya Rwanda yalifungwa kipindi cha pili
kupitia kwa Ndahinduka Michel katika dakika 55 na Meddy Kagere katika dakika ya
60 na kuipa nchi hiyo ushindi.
Rwanda walishinda penati 4-3 na Patrick Sibomana
alifunga penati ya ushindi na sasa wanaungana na mabingwa watetezi Nigeria,
Afrika kusini na Sudan katika kundi A.
0 comments:
Post a Comment