
Imechapishwa Julai 13, 2014 saa 9:52 usiku
UHOLANZI imeonesha ubora wake kwa kuipiga Brazil
mabao 3-0 jana usiku na kutwaa nafasi ya tatu ya kombe la dunia, kwa mujibu wa
kocha Louis van Gaal.
The Orange ilipata ushindi mnono dhidi ya wenyeji
na shukurani kwa mabao ya Robin Van Persie, Daley Blind na Georginio Wijnaldum,
ambapo ilikuwa mechi ya mwisho kwa Van Gaal kuiongozo Uholanzi kabla ya kuanza
kazi mpya katika klabu ya Manchester United.
Kocha huyo alisema alikuwa na furaha kuona
wachezaji wake wameimarika vizuri kufuatia kufungwa na Argentina katika mchezo
wa nusu fainali.
“Ilikuwa ngumu sana kwetu,” Van Gaal aliwaambia NOS baada ya mchezo. “Ugumu wote ulikuwa
kwetu. Brazil walikuwa angalau na siku zaidi ya maandalizi na tulifungwa kwa
penati”.
“Tungekuwa fainali. Morali yetu ilishuka baada
kufungwa na Argentina. Nitazungumzia mechi ya Brazil katika mazungumzo na timu yangu na sio kuhusu Argentina. Kwa
bahati nzuri tumeonesha tena jinsi gani tuna ubora”.
Kipa wa Swansea, Michel Vorm aliingia katika dakika ya mwisho ,
inamaanisha Uholanzi imewatumia wachezaji wote 23 katika fainali za 2014 nchini
Brazil.
“Ni ajabu kwamba tumetumia wachezaji wote 23, Van
Gaal alisema. “Wachezaji walimhitaji Vorm katika kikosi cha kwanza, lakini
niliwaambia haitawezekana kwasababu nilikuwa nahitaji kikosi bora cha kwanza.
Wakati tunaongoza 2-0 nilipata hisia nzuri za kumuingiza katika timu”.
0 comments:
Post a Comment