
Mmenisoma hapo?: Luis Suarez amekamilisha uhamisho wake wa paundi milioni 75 kutokea Liverpool kwenda Barcleona.

Karudi kazini: Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers alipigwa picha akiwa katika mazoezi yake ya kwanza ya maandilizi ya msimu siku ya jumatatu.
Imechapishwa Julai 12, 2014, saa 5:44 asubuhi
Brendan Rodgers amefunguka na kusema ataifanya Liverpool kuwa imara baada ya kumruhusu Luis Suarez kuondoka.
Kocha huyo wa Liverpool amemruhusu Suarez kwenda Barcelona baada ya wakatalunya hao kukubali kulipa dau la paundi milioni 75 na atatangazwa rasmi kama mchezaji wa Nou Camp wiki ijayo baada ya vipimo vya afya.
Msimu uliopita, Suarez alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu England na mshindi wa tuzo ya PFA na Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka inayotolewa na waandishi wa habari, hivyo kuondoka kwake imekuwa huzuni kwa mashabiki wa Liverpool.
Lakini Rodgers amewatuliza mashabiki wa majogoo wa jiji na kusema ataiboresha zaidi Liverpool, kwasababu klabu ni kubwa kuliko mtu mmoja.

Hayupo tena: Rodgers (kushoto) alisema Liverpool ilijaribu kwa kila namna kumbakisha Luis Suarez katika klabu ya Liverpool.

Amefungiwa: Luis Suarez amefungiwa miezi minne kwa kitendo cha kumng`ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini katika mechi ya fainali ya kombe la dunia.
Rodgers aliyemtetea Suarez baada ya kumng`ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic mwaka jana alisema: "Klabu imefanya kila jitihada ili kumbakisha Luis Suarez".
"Imekuwa ngumu kukubaliana baada ya majadiliano ya muda mrefu, na kwasasa tumeshakubaliana aende Hispania ili apate changamoto mpya"
Rodgers anakabiliana na changamoto ya kutafuta mbadala wa mchezaji aliyefunga mabao 31 msimu uliopita.
Mshambuliaji wa QPR, Loic Remy na wa Swansea, Wilfried Bony ndio wachezaji wanaowindwa zaidi.
Lakini Rodgers aliahidi: "Nina imani tutaimarisha timu zaidi na tutakuwa wakali zaidi msimu ujao. Kama kuna kitu cha kihistoria ambacho klabu hii inatufundisha, ni kwamba, Liverpool ni kubwa kuliko mtu binafsi. Natumaini mashabiki wetu wanaota na wanaamini kuwa tunakwenda mbele na tutaendelea kusonga zaidi, kwapamoja tutaleta mafanikio".
0 comments:
Post a Comment