
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa utaratibu utakaowawezesha washabiki
kwenda jijini Harare, Zimbabwe kushuhudia mechi ya Taifa Stars.
Mechi
hiyo ya marudiano ya Kombe la Afrika kwa ajili ya fainali zitakazochezwa
Morocco mwakani itafanyika Jumapili (Juni 1 mwaka huu) jijini Harare.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilishinda mechi ya kwanza
iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0.
Usafiri
huo utakuwa wa basi ambapo washabiki wanatarajiwa kuondoka siku ya Ijumaa na
kuwasili Jumapili mchana jijini Harare ambapo watashuhudia mechi na kuanza
safari ya kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo.
Washabiki
wanatakiwa kuwa na hati za kusafiria (pasipoti), nauli ya kwenda na kurudi
itakuwa sh. 300,000.

0 comments:
Post a Comment