MAELFU ya mashabiki wa Asernal wamefurika katika mitaa ya London kaskazini kushangalia ubingwa wa FA waliotwaa jana kwa kuwafunga Hull City mabao 3-2 baada ya kukaa miaka 9 bila taji.
Wachezaji walikuwa katika basi la wazi lililoondoka Emirates majira 11:00 asubuhi na kuzunguka mjini Islington, mitaa ya juu ya mji wa London na kurudi uwanjani.

Ukame umekwisha! Wachezaji wa Arsenal wakishangilia baada ya kumaliza ukame wao wa kukaa bila kombe

Pati! Wachezaji wa Arsenal akiwemo Aaron Ramsey (kulia), wakiwa wamebeba kombe lao mbele ya mashabiki

Mashabii wakiwapungia mikono wachezaji wao wakati wanapita na basi

Mfungaji wa goli, Laurent Koscielny akiwa amebeba kombe leo jumapili

Walianzia katika uwanja wa Emirates na kuzunguka mji wa London

Maelfu ya mashabiki wa Asernal walifurika katika mitaa ya Islington kushangilia ubingwa

Mashabiki waliofurika

Arsene Wenger akinyanyua kombe lililomfanya aamue kubakia Asernal
0 comments:
Post a Comment