


……………………………………………………………..
Dar es Salaam, Wafanyakazi wa Quality Furniture Limited jana walipatiwa mafunzo juu ya utoaji bora wa huduma kwa wateja na kampuni ya Peak Performance International Tanzania, PPIT.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Accomondia Hotel, mkuu wa mafunzo wa PPIT Bi Claudine Muthama alisema kuwa “ katika dunia ya sasa ya kibiashara ambapo ushindani ni suala la kila siku na wateja wana machaguo mengi ya bidhaa na huduma suala la huduma bora kwa wafanyakazi ni suala mtambuka.”
Aliendelea kusema maneno mazuri kwa mteja yanaweza kufanya huduma yako kusambaa kwa watu wengi zaidi maana watu wana tabia ya kusimuliana. Kwahiyo kama kampuni au mtu binafsi atakosea katika huduma kwa wateja watu hawatajikisikia kurudia biashara na wewe.
Zaidi ya hayo kazi ya huduma kwa wateja inahitaji mtu ambae ni msikivu, mwenye kusoma saikolojia ya mteja kwa haraka pia uvumilivu pale unapopata mteja mgumu kushika maelekezo.
Kwa upande wao wafanyakazi wa Quality Furniture walisifia mafunzo hayo wakisema yamewapa mwanga na kuongeza uelewa wao katika huduma bora kwa wateja ambao hawakuwa nayo hapo kabla.
“Mafunzo haya yalikuwa na lengo kubwa la kubadili mitazamo ya wafanyakazi. Tunaamini baada ya mafunzo haya leo kila mmoja wetu amepata nguvu mpya na anaenda kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kupata huduma bora.” alisema bwana Tonny Obura Meneja Mauzo na Masoko wa Quality Furniture.
Peak Performance International Tanzania, PPIT ni kampuni inayoongoza Tanzania kwa kutoa mafunzo kwa makampuni na watu binafsi juu ya huduma bora kwa wateja, ufanisi kazini, umoja na mshikamano, kutambua uwezo ulioko ndani yako pamoja na mafunzo mengine mengi yenye lengo la kuboresha na kukuza ufanisi kazini na mafanikio kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment