Watu wanne wamefariki dunia mkoani hapa katika matukio tofauti akiwamo mmoja kufa baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga wakati akichimba dhahabu na mmoja kujeruhiwa kwa kifusi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile, alimtaja aliyefukiwa na kifusi kuwa ni Lucas Charles (55), mkazi wa Kibangile tarafa ya Matombo wilayani Morogoro.
Kamanda Shilogile alimtaja aliyejeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi hicho kuwa ni Hamad Dulege (50).
Alisema tukio hilo lilitokea Desemba 22, mwaka huu saa 11:00 jioni eneo la Mfizinga kijiji cha Uponda, Tarafa ya Matombo.
Wakati huo huo, mfugaji wa jamii ya Kimasai, Matinda Kakurwa (35), mkazi wa Usungurwa Ngerengere Wilaya ya Morogoro, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kwenye chembe ya moyo na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi kisha wakampora fedha.
Alisema inadaiwa kuwa mfugaji huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, alikuwa na kiasi kikubwa cha fedha ambacho hadi sasa hakijafahamika.
Alifafanua kuwa majambazi hayo yalimvamia na kuchukua fedha hizo kisha kutokomea kusikojulikana.
Alifafanua kuwa majambazi hayo yalimvamia na kuchukua fedha hizo kisha kutokomea kusikojulikana.
Alisema tukio hilo lilitokea Desemba 22, mwaka huu saa 1:00 asubuhi katika kijiji cha Kwaba Maporini Ngerengere.
Kamanda Shilogile alifafanua kuwa katika eneo la tukio, iliokotwa risasi moja ambayo haijatumika pamoja na ganda la risasi la bunduki aina ya Riffle.
Hata hivyo, alisema hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Hata hivyo, alisema hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Aidha, Kamanda Shilogile alisema katika tukio lingine, mtembea kwa miguu, Asma Mustapha (8), mkazi wa kijiji cha Wami Sokoine Wilaya ya Mvomero, alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari isiyofahamika namba wala dereva katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma.
Na katika tukio lingine alisema mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 hadi 30, alifariki dunia baada ya kugongwa na gari lisilofahamika namba wala dereva katika eneo la Bwawa la Hatari Wami Dakawa barabara ya Morogoro – Dodoma.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment