Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha la Krismas
wametangaza viingilio vya tamasha hilo ambavyo kima cha chini ni
shilingi 5000.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama viingilio vingine viti vya kawaida, 10000 VIP B na VIP A 20000.
Msama
alisema watoto katika tamasha hilo watachangia shilingi 2000 ambako
alitoa wito kwa jamii kujipanga kwa ajili ya tamasha hilo.
Aidha
Msama alisema viingilio katika mikoa yote litakakofanyika ni shilingi
5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000na kuendelea kueleza kwamba
wadau wajipange vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo.
“Tunafanya
taratibu za tiketi za tamasha hilo ambazo tumepanga zitoke Uingereza,
ili kukwepa wizi utakaofanywa na baadhi ya wasiolitakia mema,” alisema
Msama.
Msama
alisema wanajipanga vilivyo kuhakikisha wanakomesha ujanja unaotarajia
kufanywa na wasiolitakia mema tamasha hilo ambalo dhamira yake ni
kusaidia wanaoishi katika mazingirahatarishi wakiwemo yatima, wajane na
walemavu.
Waimbaji
katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo
Kilahiro, John Lisu na New Life Band (Tanzania) na waimbaji kutoka nje
ya Tanzania ni pamoja na Solly Mahlangu, Liliane Kabaganza, Solomon
Mukubwa na Eiphraim Sekeleti.


0 comments:
Post a Comment