Kaimu
Mkurugenzi Mkuu toka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Hamza
Kabelwa akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) ramani ya
Mwelekeo wa msimu wa mvua za October hadi December 2013,ambapo rangi ya
njano katika picha inaashiria mvua za wastani na rangi ya kijani
inaashiria mvua za chini ya wastani. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa
Mamlaka hiyo Bi.Monica Shayo

Kaimu
Mkurugenzi Mkuu toka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Hamza
Kabelwa akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mikakati ya
Serikali katika kuendeleza huduma za hali ya hewa katika sekta ya
usafiri wa baharini,Visiwani Zanzibar na katika maziwa nchini,wakati wa
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini
Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi.Monica
Shayo.

Kaimu
MkurugMamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Hamza Kabelwa
akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) cheti cha utambuzi
walichopokea kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya
Usafiri Baharini(ZMA) kutokana na kuutambua mchango wao katika usafiri
wa Baharini.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bi.
Georgina Misama.
Picha na Hassan Silayo- MAELEZO
Serikali yazidi kuboresha huduma za hali ya hewa katika sekta ya usafiri wa baharini visiwani Zanzibar na katika maziwa nchini.
Katika
jitihada za kupunguza maafa na kuhakikisha kuwa huduma za hali ya hewa
nchini zinazidi kuwa bora, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imefungua
kituo cha huduma za hali ya hewa kwa watumiaji wa usafiri wa baharini.
Ofisi hiyo ilianzishwa rasmi tarehe 28/04/2013 katika bandari ya
Zanzibar, ikiwa na lengo la kuhakikisha taarifa za hali ya hewa kwa
usafiri wa baharini zinapatikana na ushauri unatokewa kwa watumiaji kwa
wakati, hapo awali huduma hizi zilikuwa zinaandaliwa na kutolewa kutoka
ofisi za hali ya hewa zilizopo kituo kikuu cha utabiri – Dar es Salaam
na uwanja wa ndege wa Karume – Zanzibar.
Kwa
upande wa usafiri katika maziwa, Mamlaka imenunua mtambo mkubwa wa
kuchambua taarifa za hali ya hewa (computer cluster) utakaowezesha
huduma za hali ya hewa kutolewa katika maziwa yote makuu hapa nchini.
Katika
kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA),
iliipatia Mamlaka ya Hali ya Hewa cheti cha kuutambua mchango huo
(Certificate of Appreciation) kwa kutambua mchango wa Mamlaka katika
usafiri wa baharini.
Vilevile,
Mamlaka kupitia ofisi ya Zanzibar ilitunikiwa cheti cha kuutambua
mchango wake katika kukabiliana na maafa (Certificate of Appreciation).
Cheti hicho kilitolewa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais SMZ, Kitengo
cha Maafa.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
0 comments:
Post a Comment