Mkutano kazi kwa njia ya Mtandao ukiendelea: Sehemu ya washiriki wa mkutano kama wanavyoonekana katika kioo cha Runinga “Screen“,
picha kubwa ni Mkoa wa Ruvuma na picha ndogo ni mikoa ya Mara, Ruvuma,
na Shinyanga ambapo mawasiliano ni ya moja kwa moja, ikijumuisha picha
na sauti.
Mmoja
wa washiriki wa mkutano kazi baina ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na watenda kutoka mikoa ya Rukwa, Ruvuma, Mara na
Shinyanga akiuliza swali. Picha ndogo kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HABB Mkwizu akisikiliza
maswali.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akifungua kikao kazi kwa njia ya mtandao “Video Conference” kilichowakutanisha watendaji kutoka mikoa ya Mara, Rukwa, Ruvuma na Shinyanga
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeendesha mkutano kazi kwa njia ya mtandao “Video Conference”
na Wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa wa Mikoa ya Mara, Rukwa,
Ruvuma na Shinyanga. Mkutano huo umewakutanisha kwa pamoja watendaji
hao moja kwa moja wakiwa katika ofisi zao bila kuingia gharama za
kusafiri nje ya vituo vyao vya kazi, hivyo kuokoa rasilimali fedha na
muda ili kutoa huduma kwa wananchi.
Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB
Mkwizu amesema mikutano hiyo itaendelea kwa mikoa yote hapa nchini
kushirikishwa, ambapo watendaji kutoka mikoa hiyo watapata fursa ya
kuuliza maswali mbalimbali wanayokabilina nayo katika utendaji kazi
katika Utumishi wa Umma.

0 comments:
Post a Comment