Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI
wa Tamasha la Krismas wameeleza kuwa mashabiki wengi nchini wameomba
Malkia wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope, awepo
kwenye tamasha mwaka huu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema mwishoni
mwa wiki kuwa wamekuwa wakipokea maombi mengi kutoka kwa wadau hao
kuhusiana na ujio wa Malope, ambaye amewahi pia kuja nchini kutumbuiza
kwenye Tamasha la Pasaka.
“Homa
ya Tamasha la Krismas imeanza kupanda, mashabiki wamekuwa wakiomba
safari hii tusiache kumualika Malope, yapo maombi mengi lakini hilo la
Malope linaongoza kwamba lazima awepo tamasha la Krismas Dar es Salaam,”
alisema Msama.
Rebecca
amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009),
Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at
Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits
(Januari 10, 2006).
Tamasha la Krismas linaloandaliwa na Kampuni
ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha
la Pasaka kila mwaka linatarajiwa kufanyika Desemba 25 mwaka huu jijini
Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Msama, Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismas imeamua
lifanyike Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Desemba 25 na siku inayofuata
watatazama mkoa gani waupe heshima.
Alisema
hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na
tofauti kubwa iilinganisha na matamasha mengine yaliyowahi kuandaliwa na
kampuni yake.
Cio…
0 comments:
Post a Comment